Pata taarifa kuu
MAURITANIA-UCHUNGUZI

Raia wa Mauritania kutoweka Mali: Wataalamu wa Mauritania wazuru Bamako

Ujumbe wa wataalam wa Mauritania uko mjini Bamako tangu Jumatano jioni kushiriki katika ujumbe wa kujaribu kufafanua tukio la hivi karibuni la kutoweka kwa Wamauritania kadhaa nchini Mali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Mauritania imetangaza.

Waendesha ngamia wa kikosi cha kuhamahama kutoka vikosi vya  usalama vya Mauritania kwenye mpaka na Mali.
Waendesha ngamia wa kikosi cha kuhamahama kutoka vikosi vya usalama vya Mauritania kwenye mpaka na Mali. © Mounia Daoudi/RFI
Matangazo ya kibiashara

Kuwasili kwa ujumbe huu wa Mauritania - unaoundwa na wanajeshi na askari, kwa mujibu wa chanzo cha usalama - kunakuja baada ya Mali na Mauritania kukubaliana siku ya Jumamosi kujaribu kufafanua tukio la kupotea kwa watu hao kwa kuanzisha ujumbe wa pamoja.

Tukio hilo lilisababisha hali ya wasiwasi huko Nouakchott wakati ambapo utawala wa kijeshi nchini Mali, chini ya shinikizo la kimataifa,ulikuwa ukijaribu kuimarisha uhusiano.

Serikali ya Mali ilituma ujumbe unaoongozwa na Waziri wake wa Mambo ya Nje Abdoulaye Diop kwenda Nouakchott siku ya Ijumaa na Jumamosi ili kujaribu kutuliza mamlaka ya Mauritania.

Viongozi wa mapinduzi wametaka kukabiliana na vikwazo vilivyowekwa mwezi Januari na Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS, kuidhinisha mpango wao wa kusalia madarakani kwa miaka kadhaa zaidi. Mauritania, ambayo si sehemu ya ECOWAS, imeweka mpaka wake wazi.

"Katika eneo la tukio, wataalam wataanza kazi yao kulingana na kile kilichoamuliwa wakati wa mkutano wa wajumbe wawili wa ngazi ya juu mnamo Machi 12, 2022 huko Nouakchott", inabainisha taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Mauritania iliyotolewa Jumatano jioni.

Ujumbe wa pamoja una jukumu la "kuanzisha uchunguzi kuhusiana na ajali mbaya ya Machi 5 na kuzuia mashambulizi dhidi ya raia wa Mauaritania na mali zao", kulingana na nakala hiyo.

Mauritania ilikuwa imepaza sauti yake dhidi ya jirani yake Machi 8, ikilishutumu jeshi lake kwa "vitendo vya uhalifu vya mara kwa mara" katika ardhi yake dhidi ya Wamauritania, kufuatia kutoweka watu kadhaa katika eneo la mpaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.