Pata taarifa kuu

Mauritania yapandwa na hasira baada ya raia wake kutoweka kwenye mpaka na Mali

Kumeibuka vutano kati ya Mauritania na Mali, kufuatia kutoweka kwa wafugaji wa Mauritania katika ardhi ya Mali. Dazeni kadhaa za raia wa Mauritania wametoweka kwa takriban siku tatu.

Mji mkuu wa Mauritania, Nouakchott.
Mji mkuu wa Mauritania, Nouakchott. GEORGES GOBET / AFP
Matangazo ya kibiashara

Duru za ndani zinasema kuwa waliuawa na wanajeshi wa Mali, madai ambayo bado hayajathibitishwa. Eneo la mpakani kati ya nchi hizo mbili limekuwa linakabiliwa na ongezeko la machafuko kwa wiki kadhaa.

Mamlaka ya Mauritania inasema imeghadhabishwa na visa hivyo. Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa Jumanne mchana, Wizara ya Mambo ya Nje inalishutumu jeshi la Mali "kwa uhalifu wa mara kwa mara dhidi ya raia wake". Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, wizara hiyo pia inabaini kwamba maisha ya raia wa Mauritania yatasalia juu ya jambo lingine lolote, wakati mamlaka ya Mali imefanya maelewano na Nouakchott, kufuatia vikwazo vilivyowekwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS.

Saa chache mapema, katibu mkuu kwenye wizara ya Mambo ya Nje alimpokea balozi wa Mali. "Tunapigia simu viongozi wenu huko Bamako, lakini hawapokei," afisa huyu amesikitishwa wakati mazungumzo, kulingana na chanzo cha kidiplomasia huko Nouakchott.

Jumatatu jioni, Wizara ya Mambo ya Ndani ilielezea wasiwasi wake, na kuahidi kutoa mwanga juu ya hatima ya waliotoweka.

Tukio la tatu la aina hiyo katika miezi miwili

Watu kadhaa pia waliandamana Jumanne mchana mbele ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Mauritania. Kwenye mabango waliandika "uchokozi wa jeshi la Mali".

Ninaamua kupaza sauti. Hili lazima ikome. Hatuwezi tena kukubali kwamba wazazi wetuwafanyie madhila na jeshi la Mali. Mauaji haya ya mara kwa mara lazima yakome.

Hili ni tukio la tatu linalohusiana na usalama kuwakumba raia wa Mauritania nchini Mali katika kipindi cha miezi miwili. Siku ya Jumamosi, wafanyabiashara wawili walipigwa risasi na kujeruhiwa walipokuwa wakirejea Abel Bagrou, mji wa mpakani. Mnamo Januari 17, miili ya wafugaji saba ilipatikana karibu na kijiji cha Mali cha Nara. Baada ya maandamano kutoka Nouakchott, mamlaka ya Mali iliahidi uchunguzi juu ya tukio hili, lakini ikahakikisha kwamba hakuna kinachoruhusiwa kushutumu vikosi vyao vya kijeshi. Maelezo ya uchunguzi huu bado hayajatangazwa kwa umma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.