Pata taarifa kuu

Wafanyabiashara saba wa Mauritania wauawa katika ardhi ya Mali

Mvutano mkubwa umeibuka kwenye mpaka wa Mauritania na Mali, baada ya mauaji ya wafanyabiashara 7 wa Mauritania katika nchini Mali. Tukio lilitokea karibu na mji wa Nara Jumatano wiki hii, Januari 19.

Mali na Mauritania zinachangia mpaka mrefu.
Mali na Mauritania zinachangia mpaka mrefu. RFI
Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya rais wa Mauritania inasikitishwa na tukio hili la huzuni lililogharimu maisha ya raia 7 wa Mauritania. Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa ofisi ya rais haielezei utambulisho wa wahanga hawa, wala sababu za kuuawa kwao.

Lakini jeshi la Mali linahusika katika mauaji haya, kulingana na shuhuda zilizokusanywa kutoka kwa familia za wahanga na mashirika ya habari ya mtandaoni ikiwa ni pamoja na Alakhbar.

Mkuu wa Nchi ya Mauritania Mohamed Ould Cheikh Ghazouani aliwatuma Bamako Mawaziri wa Mambo ya Nje, Ulinzi wa Taifa, Mambo ya Ndani na Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa.

Uchunguzi sasa utalazimika kubaini mazingira ya tukio hilo la kusikitisha na waliohusika. Adhabu kali zaidi zitatolewa kwa wahusika wa uhalifu huo, mamlaka imesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.