Pata taarifa kuu

Mali yatoa heshima ya kitaifa kwa IBK na kuanza kwa maombolezo ya kitaifa ya siku 3

Nchini Mali, Viongozi na raia mbalimbali wanatoa heshima ya kitaifa Ijumaa hii, Januari 21, kwa rais wa zamani Ibrahim Boubacar Keïta, aliyefariki Jumapili iliyopita huko Bamako. Maombolezo ya kitaifa ya siku tatu kuanzia Ijumaa hii yametangazwa na rais wa mpito, kanali Assimi Goïta. Mambo mawili muhimu yanatangazwa kwa siku hiyo: sherehe ya heshima na maziko ya IBK ambayo yatasimamiwa na kufanywa na familia.

Rais wa zamani wa Mali, hapa ilikuwa mwaka2020, atazikwa Ijumaa hii Januari 21 katika makazi yake ya Sébénikoro huko Bamako, na heshima ya kitaifa inatolewa kwake.
Rais wa zamani wa Mali, hapa ilikuwa mwaka2020, atazikwa Ijumaa hii Januari 21 katika makazi yake ya Sébénikoro huko Bamako, na heshima ya kitaifa inatolewa kwake. Issouf Sanogo/AFP
Matangazo ya kibiashara

Keita, anayejulikana pia kama IBK, aliongoza nchi hiyo ya Afrika Magharibi kuanzia Septemba 2013 hadi Agosti 2020, kipindi cha misukosuko ambacho kilishuhudia uasi mkali wa Kiislamu ukichukua maeneo makubwa ya kaskazini na kati na kupelekea kupoteza umaarufu wake.

Ibrahim Boubacar Keïta alikuwa Waziri Mkuu kuanzia mwaka 1994 hadi mwaka wa 2000 chini ya utawala wa Oumar Konaré. Kisha alishindwa katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2002. Lakini hatimaye alichaguliwa na kufika Ikulu ya Koulouba, makao makuu urais wa Mali huko Bamako, mwaka wa 2013. Alichaguliwa tena mwaka wa 2018 dhidi ya Soumaïla Cissé, kiongozi wa upinzani wakati huo, ambaye alifariki dunia mwezi Desemba 2020 kwa ugonjwa wa Covid-19.

Alilazimishwa kutoka madarakani na mapinduzi ya kijeshi baada ya miezi kadhaa ya maandamano dhidi ya serikali. alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 76.

Rais wa zamani wa Mali atazikwa Ijumaa hii Januari 21 katika makazi yake ya Sébénikoro huko Bamako.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.