Pata taarifa kuu

Rais wa zamani wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta afariki dunia

Rais wa zamani wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta, ambaye aliongoza Mali kati ya mwaka 2013 na 2020, amefariki dunia Jumapili Januari 16 nyumbani kwake mjini Bamako, kulingana na familia yake. Ibrahim Boubacar Keïta, aliyechaguliwa kuwa rais wa Mali mmwezi Septemba 2013, alipinduliwa na wanajeshi mwezi wa Agosti 2020.

Rais a zamani wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita.
Rais a zamani wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita. Ludovic Marin /Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Ilikuwa saa tatu asubuhi Jumapili Januari 16, wakati rais, anayefahamika kwa jina la IBK, alipofariki dunia, amesema mmoja kati watu wa familia ya Ibrahim Boubacar Keita. Karibu saa saba na nusu mchana, hakukuwa na watu wengi nyumbani yake, lakini watu walikuwa wakielekea nyumbani kwake kutoa rambirambi zao. Wasaidizi wake wa zamani, hasa mkurugenzi kwenyeofisi yake, pia amethibitisha kifo chake.

Inajulikana kwamba alikuwa mgonjwa hivi majuzi, baada ya mapinduzi ya Agosti 18, 2020. Alitibiwa mara kadhaa huko Abu Dhabi katika hospitali inayomilikiwa na Marekani. Mtu aliyemwona hivi karibuni alisema hivi, siku chache zilizopita: "Rais anakaribia kufariki dunia." Hakuwa na hamu ya kula. Hakuweza kusoma tena, mnajua kuwa alikuwa akipenda kusoma sana vitabu na waandishi.

Ibrahim Boubacar Keïta alikuwa Waziri Mkuu kuanzia mwaka 1994 hadi mwaka wa 2000 chini ya utawala wa Oumar Konaré. Kisha alishindwa katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2002. Lakini hatimaye alichaguliwa na kufika Ikulu ya Koulouba, makao makuu urais wa Mali huko Bamako, mwaka wa 2013. Alichaguliwa tena mwaka wa 2018 dhidi ya Soumaïla Cissé, kiongozi wa upinzani wakati huo, ambaye alifariki dunia mwezi Desemba 2020 kwa ugonjwa wa Covid-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.