Pata taarifa kuu
MALI-VIKWAZO

Baraza la Usalama la UN lagawanyika kuhusiana na vikwazo dhidi ya Mali

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana na Jumanne, Januari 11, kuhusu hali ya Mali na wajumbe katika mkutano huo waligawanyika kuhusiana na vikwazo vilivyochuliwa dhidi ya nc hiyo ya Afrika.

Jumanne hii, vikwazo vilivyotangazwa na ECOWAS dhidi ya Mali vilikuwa kwenye ajenda ya mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Jumanne hii, vikwazo vilivyotangazwa na ECOWAS dhidi ya Mali vilikuwa kwenye ajenda ya mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. © Timothy A. Clary, AFP
Matangazo ya kibiashara

Nchi za Afrika na Ufaransa zilitaka baraza hilo kukutana ili kupitisha msimamo wa pamoja kuelekea jeshi lililo madarakani nchini Mali. Na kwamba jumuiya ya kimataifa iunge mkono Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, ambayo ilichukuwa vikwazo vipya dhidi ya Bamako, baada ya utawala wa kijeshi kupinga kufanyika kwa uchaguzi kama ilivyoahidiwa. Lakini Urusi na China zilizuia rasimu ya tamko hilo.

Katika mkutano huo, mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Mali alitoa taarifa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuwakumbusha wanachama 15 kuhusu mazingira ambayo mashauriano ya kitaifa yalifanyika na hitimisho lao, tangazo la mamlaka ya mpito kuahirisha uchaguzi wa rais hadi mwisho wa mwaka wa 2026, majibu ya ECOWAS na vikwazo vilitangazwa siku chache baadae.

Kwa upande wake, anaona kuwa Braza la Usalama la Umoja wa Mataifa litaendelea kufanya kazi pamoja na mamlaka ya Mali, ECOWAS na Umoja wa Afrika, AU, ili kuondokana na mkwamo huo. Walinda amani 1,000 wa ziada wa Chad waliokubaliwa na Bamako wanapaswa kuwezesha hali ya mambo kubadilika. Lakini Umoja wa Mataifa na wajumbe wa Baraza wamelalamika kuhusu kuzorota kwa hali ya usalama nchini Mali, wakikumbusha walinda amani 28 waliouawa mwaka 2021, ameripoti mwandishi wetu mjini New York, Carrie Nooten.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.