Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-VIKWAZO

Vikwazo vya ECOWAS dhidi ya Mali vyasababisha msukosuko wa kisiasa Côte d’Ivoire

Vikwazo vilivyowekwa na ECOWAS dhidi ya utawala wa Mali vinasababisha msukosuko wa kisiasa nchini Côte d'Ivoire. Saa chache baada ya kutangazwa kwa vikwazo hivyo, baada ya kuandamana na kuwaita mabalozi wake katika eneo hilo, Mali ilimwachilia huru balozi wa zamani wa Soroist ambaye aliombwa na mahakama ya Ulaya kumrejesha nyumbani. Hata hivyo, Chama cha Laurent Gbagbo kimejitokeza na kushutumu vikwazo hivi.

Chama kipya cha Pan-Africanist cha Laurent Gbagbo "kinaona hatua za kulipiza kisasi zilizochukuliwa na ECOWAS dhidi ya raia wa Mali kuwa ni nyingi na zisizofaa".
Chama kipya cha Pan-Africanist cha Laurent Gbagbo "kinaona hatua za kulipiza kisasi zilizochukuliwa na ECOWAS dhidi ya raia wa Mali kuwa ni nyingi na zisizofaa". © AP - Diomande Ble Blonde
Matangazo ya kibiashara

Chama kipya cha Pan-Africanist cha Laurent Gbagbo "kinaona hatua za kulipiza kisasi zilizochukuliwa na ECOWAS dhidi ya raia wa Mali kuwa ni nyingi na zisizofaa". Katika taarifa iliyotiwa saini na msemaji wake Justin Koné Katinan, PPA-CI pia mekitaja kile alichokiita "kutokubalika na hatari" kwa kile anachokichukulia kama "kutumiwa kwa taasisi za fedha na benki za jumuiya kutatua masuala ya ndani ya kisiasa".

Ishara kwamba uhusiano ulidorora Jumapili jioni kati ya Mali na majirani zake, utawaa wa kijeshi wa nchi hiyo uliwaita nyumbani mabalozi wake katika ukanda huo. Na siku ya Jumatatu mjini Bamako, mbunge wa zamani anayemuunga mkono Soro, Sess Soukou Mohamed, anayejulikana kwa jina la Ben Souk aliachiliwa ghafla, usiku wa kuamkia siku yake ya kusikilizwa na jaji.

Ben Souk alikamatwa Agosti 10 na kusafirishwa kwenda Côte d'Ivoire. Ben Souk pia alihukumiwa kifungo cha miaka 20 bila kuwepo mahakamani mwezi Juni kwa "kuhatarisha usalama wa mamlaka ya serikali" na "kula njama". Kesi ambayo ilimfanya Guillaume Soro ahukumiwe bila kuwepo kwa kifungo cha maisha.

Guillaume Soro alikaribisha kuachiliwa kwa mshirika wake wa kisiasa katika taarifa ambayo "alionesha uungwaji wake mkono wa dhati kwa mamlaka ya mpito" bila hata hivyo kutoa maoni yake kuhusu vikwazo.

Mtu mwingine maarufu ambaye alighadhabishwa na vikwazovya ECOWAS ni mwanamuziki nguli wa mitindo ya Reggae, Alpha Blondy.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.