Pata taarifa kuu

Raia wa Mali wamiminika tena mitaani kupinga vikwazo vya ECOWAS

Maelfu ya raia wa Mali, kwa mara nyingine wamekuwa wakiandamana jijini Bamako, kulaani hatua ya nchi za Jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, kuiwekea vikwazo vya kiuchumi baada ya pendekezo la serikali ya mpito iendelee kusalia madarakani kwa miaka mitano.Β 

Watu wakiandamana katika mitaa ya mjini Bamako kupinga vikwazo vipya vilivyowekwa dhidi ya Mali kutokana na utawala wa kijeshi kuchelewesha uchaguzi.
Watu wakiandamana katika mitaa ya mjini Bamako kupinga vikwazo vipya vilivyowekwa dhidi ya Mali kutokana na utawala wa kijeshi kuchelewesha uchaguzi. FLORENT VERGNES AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Maandamano haya yanakuja wakati huu Umoja wa Afrika kupitia Baraza la amani na usalama, likitoa taarifa ya kuunga mkono vikwazo hivyo vya kiuchumi vilivyowekwa na ECOWAS.Β 

Hata hivyo, Umoja wa Afrika unasema nchi ya Mali ianze haraka mchakato wa Uchaguzi na kuhakikisha kuwa unafanyika ndani ya miezi kumi na sita.Β 

Umoja wa Afrika unasema pendekezo la uongozi wa jeshi kusalia madarakani kwa miaka mitano kabla ya kuandaa uchaguzi huo, haikubaliki, ni kinyume cha katiba na inarudisha nyuma mchakato wa demokrasia nchini Mali.Β 

Aidha, Umoja huo unataka uongozi wa jeshi kuwaachia huru wafungwa wote wa kisiasa na waliokuwa viongozi wa serikali ya mpito iliyopita akiwemo aliyekuwa Waziri Mkuu Soumeylou Boubeye MaΓ―ga na aliyekuwa Waziri wa uchumi BouarΓ© Fily Sissoko.Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.