Pata taarifa kuu

Ndege ya kijeshi ya Ujerumani yakataliwa kuruka juu ya anga ardhi ya Mali

Mali imeikatalia ndege ya jeshi la Ujerumani iliyokuwa ikienda Niger kuruka juu ya anga ya ardhi yake, jeshi la anga la Ujerumani limesema Alhamisi wiki hii.

Mwanajeshi akitembea mbele ya gari la kivita kwenye barabara ya lami kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Modibo-Keita huko Bamako, Machi 29, 2012.
Mwanajeshi akitembea mbele ya gari la kivita kwenye barabara ya lami kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Modibo-Keita huko Bamako, Machi 29, 2012. © AP - Rebecca Blackwell
Matangazo ya kibiashara

Ndege ya Bundeswehr Airbus A400M kutoka Ujerumani "ikiwa na takriban wanajeshi 80 ilinyimwa haki ya kuruka juu ya anga ardhi ya Mali ilipokuwa ikielekea Niamey, Niger," jeshi limesema, kwa mujibu wa tovuti ya VOA Afrique.

"Ndege hiyo ilielekezwa Gran Canaria", katika Visiwa vya Canary (Uhiispania), limebainisha jeshi, likionya kwamba "ukweli utawekwa wazi".

Mamlaka ya Mali hivi majuzi ilizuia safari za ndege za ujumbe wa kijeshi wa kimataifa wa Minusma, ulioko nchini humo na ambao Ujerumani inashiriki.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani alidokeza siku ya Jumatatu kuwa Mali imepiga marufuku safari nyingi za ndege za MINUSMA tangu Alhamisi ya wiki iliyopita, zikiwemo  ndege zisizo na rubani.

Takriban wanajeshi elfu moja wa Bundeswehr wanafanya kazi katika kikosi cha na MINUSMA nchini Mali.

Viongozi wa mapinduzi walioko madarakani mjini Bamako tangu mwezi Agosti 2020 walifunga mipaka yao kwa nchi za jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, baada ya nchi hizo kufanya vivyo hivyo mwanzoni mwa mwezi Januari kuwekea vikwazo mpango wa kijeshi wa kusalia madarakani kwa miaka kadhaa bila uchaguzi.

Tangu Januari 12, swali limekuwa likiibuliwa kuhusu uhuru wa kusafiri kwa ndege za kijeshi zinazoingia au kutoka katika anga hiyo kutoka au kwenda katika mataifa ya Afrika Magharibi yanayohusika, kuanzia zile za jeshi la Ufaransa na MINUSMA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.