Pata taarifa kuu

Mali kufungua uchunguzi kuhusu tuhuma za kutoweka kwa raia wa Mauritania

Serikali ya Mali ilijibu Jumatano hii, Machi 9 kwa shutuma za serikali ya Mauritania juu ya kutoweka kwa Wamauritania nchini Mali. Katika hatua hii, inasema taarifa rasmi, "hakuna ushahidi unaohusisha Wanajeshi wa Mali", Fama. "Uchunguzi utafunguliwa", imeongeza mamlaka nchini Mali.

Oualata, Mauritania.
Oualata, Mauritania. © Mounia Daoudi/RFI
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne, katika taarifa kwa vyombo vya habari, serikali ya Mauritania ilipaza sauti dhidi ya jirani yake Mali, ikiLishutumu jeshi lake kwa uhalifu wa "mara kwa mara" katika ardhi yake dhidi ya raia wa Mauritania. Wizara ya Mambo ya Nje ya Mauritania pia ilimwita Balozi wa Mali ili kumueleza "huzuni ilionao". Dazeni kadhaa za raia wa Mauritania wametoweka kwa siku kadhaa na duru za ndani zinasema waliuawa na wanajeshi wa Mali.

Rais wa Mpito wa Mali na rais wa Mauritania wamefanya mazungumzo ya simu. Kanali Assimi Goïta ameonyesha masikitiko yake kwa mwenzake Mohamed Ould Ghazouani juu ya hatima ya raia "waliotoweka" wa Mauritania, lakini, katika hatua hii, taarifa ya serikali ya Mali inabainisha "hakuna ushahidi unaohusisha Jeshi la Mali (Fama) ambalo linaheshimu haki za binadamu na siku zote linafanya kazi kwa weledi katika mapambano yake dhidi ya ugaidi”.

Kulingana na vyanzo kadhaa vya ndani, wanajeshi wa Mali, Fama, wametumwa Magharibi mwa nchi hiyo, "kulinda" mpaka na Mauritania.

Baadhi ya wafanyabiashara au wafugaji wanaeleza kuwa aina za njia za kupita zimeanzishwa ili kuwaruhusu kwenda upande wowote wa mpaka. Vyanzo vinazungumza juu ya vituo vya ukaguzi kati ya Timbuktu na Nara. Na itakuwa hatari kwenda nje ya njia hizi zilizotangazw.

Uwepo wa wanajeshi wa kigeni

Wanajeshi wa Mali hawako peke yao katika eneo hili kwani wanasaidiwa na mshirika wao mpya, kampuni ya kibinafsi ya Urusi ya Wagner. Vyanzo kadhaa kwenye eneo hilo vimetaja kuwa wameona watu weupe wakizungumza Kirusi. Vyanzo viwili vya usalama vya Ufaransa katika eneo hilo vimethibitishia habari hii.

Mnamo Machi 1, mamluki kadhaa wa Urusi wakiandamana na wanajeshi wa Mali walikwenda Nampala, sio mbali na mpaka wa Mauritania. Kulifanyika mashambulizi, na kusababisha, kulingana na habari za kijasusi za Ufaransa, vifo vya raia thelathini na kusababisha watu kuhama makazi yao.

Kulingana na habari zetu, mamluki 1,000 kutoka kampuni ya Urusi ya Wagner wapo katika ardhi ya Mali. Katika mwezi wa Machi, ndege mbili za Urusi kutoka Libya zilileta wapiganaji wapya.

Uchunguzi wafunguliwa

Kwa upande wa Mali wanasema, vitendo hivi vya uhalifu vinakusudiwa kuzorotesha zaidi uhusiano wa kiutendaji kati ya nchi hizo mbili. Hii ndiyo sababu uchunguzi umefunguliwa kwa upande wa Mali ili kufafanua hali hiyo, inabainisha taarifa hiyo rasmi kwa vyombo vya habari. Na mamlaka ya Mali imeahidi kutafuta wahalifu wa uhalifu huu unaoelezewa kama "mbaya", ili kuwafikisha mbele ya mahakama husika.

Bamako inakusudia kwa haki haraka kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika uwanja wa usimamizi wa mipaka yao ya pamoja, lakini pia katika nyanja za ulinzi na usalama wa bidhaa na watu. Ujumbe wa kiwango cha juu wa Mali utaenda Nouakchott hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.