Pata taarifa kuu
USALAMA-SIASA

Usalama, moja ya changamoto nyingi zinazomubiri Rais mpya wa Nigeria Tinubu

Kuibuka tena kwa mashambulizi makubwa ya makundi ya wahalifu na wapiganaji wa kijihadi nchini Nigeria, wakati uliopunguza kasi wakati wa kipindi cha uchaguzi, ni ukumbusho muhimu wa changamoto kubwa zinazomsubiri Bola Tinubu ,rais mteule wa Nigeria, nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika, kuanzia Jumatatu ya wiki inayokuja.

Bola Tinubu baada ya kuchaguliwa kwake kama rais wa Nigeria mnamo Machi 1, 2023.
Bola Tinubu baada ya kuchaguliwa kwake kama rais wa Nigeria mnamo Machi 1, 2023. AP - Ben Curtis
Matangazo ya kibiashara

Vurugu hizi pia ni kielelezo kikali cha kushindwa kwa Rais anaye maliza muda wake Muhammadu Buhari, jenerali wa zamani wa mapinduzi katika jeshi, ambaye alichaguliwa kidemokrasia mwaka 2015 na 2019 kwa ahadi ya kuleta amani nchini Nigeria.

Kwa sababu hakuna wiki, hakuna siku inayopita bila kuripotiwa mashambulizi makubwa ya makundi ya wahalifu (kaskazini-magharibi na katikati), wanajihadi (kaskazini-mashariki), au wanaharakati wanaotaka kujitenga kwa maeneo yao (kusini-mashariki) na hivyo kusababisha vifo vingi kuripotiwa, wakati Nigeria ni mojawapo ya nchi zenye nguvu zaidi barani Afrika.

Mara kwa mara na nguvu zao zilitishia uchaguzi wa urais, wa wabunge na wa serikali za mitaa wa mwezi Februari na Machi mwaka huu. Hali ya utulivu iliyoonekana wakati wa kipindi cha uchaguzi ilishangaza kila mtu, na kuruhusu kufanyika kwa chaguzi hizi, hata katika maeneo yenye hali tete. Iliwezesha kuchaguliwa kwa Bola Tinubu, ambaye ataapishwa siku ya Jumatatu, ingawa matokeo yanapingwa mahakamani na upinzani, ambao unashutumu udanganyifu mkubwa uliofaywa na chama tawala.

Hata hivyo, utulivu huu ulikuwa wa muda mfupi, kwa sababu kutoka mwezi Aprili milio ya risasi ilianza tena kusikika kwa nguvu kubwa zaidi. Kwa muda wa miezi miwili, orodha ya mashambulizi inaonekana kutokuwa na mwisho: zaidi ya watu 100 wamepoteza maisha na 3,000 wamekimbia makazi yao baada ya mapigano kati ya jamii, waumini 25 kutekwa nyara kanisani, askari 5 waliuawa katika mlipuko wa bomu la kutegwa ardhini ...

"Mara tu atakapoingia madarakani, rais mpya atakabiliwa na matatizo makubwa ya kiusalama," anabainisha Emeka Okoro, mchambuzi wa masuala ya usalama wa kundi la uchanganuzi la SBM Intelligence, na atalazimika kukabiliana na nyanja tatu kuu.

Jambo la dharura na linalopewa kipaumbele zaidi ni lile la kati na kaskazini magharibi mwa Nigeria, kulingana na Bw. Okoro. Katika maeneo haya ya kilimo na maskini, ushindani mkali wa ardhi mara kwa mara hubadilika na kuwa makabiliano makali kati ya wakulima na wafugaji, ambapo kukosekana kwa haki na ulinzi kutoka kwa mamlaka kumechangia kuzaliwa kwa magenge yenye silaha, yanayohusika na mauaji ya halaiki na utekaji nyara kwa ajili ya fidia. Jeshi linasema kuwa linafanya operesheni dhidi ya "majambazi" hao, lakini matokeo yanashindwa kuonekana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.