Pata taarifa kuu

Nigeria: Bola Tinubu atoa wito wa mshikamano

NAIROBI – Rais mteule wa wa Nigeria Bola Tinubu ametoa wito kwa wapinzani wake kuungana naye kwa ajili ya ujenzi wa taifa, baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa urais uliompa ushindi. 

Bola Tinubu, Rais Mteule wa Nigeria
Bola Tinubu, Rais Mteule wa Nigeria © AP - Ben Curtis
Matangazo ya kibiashara

“Kwa wale ambao hawakuniunga mkono,  msikubali masikitiko  hayo yawanyime fursa ya sisi kufanya kazi pamoja, ni lazima tuungane pamoja ilikupeleka nchi yetu mbele, naweza kuwa rais lakini nawahitaji zaidi, na raia wa Nigeria wanawahaitajhi hata zaidi.”amesemaBola Tinubu

Ametoa kauli hii, wakati huu wagombea wakuu wa upinzani wakiendelea kukataa kutambua ushindi wake, huku Peter Obi aliyeibuka katika nafasi ya tatu, chama chake cha Leba, kikisema kitakwenda Mahakama, kupinga ushindi wa Tinubu, wakati huu kikitoa wito wa utulivu kwa wafuasi wake. 

Wakati akipokezwa cheti chake cha rais mteule wa Nigeria, ameahidi kufanya kazi usiku na mchana kwa manufa ya raia wote wa Nigeria pamoja na kuifanya nchi hiyo kuwa bora tena.

Muhammadu Buhari rais anayemaliza muda wake, amemtaja mrithi wake Bola Tinubu kama mtu anayestahili kuliongoza taifa hilo baada yake kuondoka, Buhari akieleza kuwa ana imani na Tinubu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.