Pata taarifa kuu

Bola Tinubu ndiye rais Mteule wa Nigeria

NAIROBI – Nchini Nigeria, Tume ya uchaguzi imemtangaza Bola Tinubu mgombea wa chama tawala APC kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumamosi iliyopita.

Bola Ahmed Tinubu, Rais Mteule wa Nigeria
Bola Ahmed Tinubu, Rais Mteule wa Nigeria © daily trust
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Mahmood Yakubu amemtangaza Tinubu mwenye umri wa miaka 70, mshindi, baada ya kupata kura Milioni 8 na Laki Saba, na kuwashinda wapinzani wake wa karibu, Atiku Abubakar wa chama kikuu cha upinzani PDP aliyepata kura Milioni 6 na Laki Tisa, huku Peter Obi wa chama cha Leba, akipata kura Milioni 6.1.

“Hii sio hatua ndogo kishtoria, ni hatua kubwa sana ya mafanikio.”amesema Bola Tinubu, rais mteule wa Nigeria.

00:12

Bola Tinubu, Rais Mteule wa Nigeria

Wakati wafuasi wa chama tawala wakisherehekea ushindi huu, vyama vya upinzani vimeyakataa matokeo hayo kwa kile wanachosema, Tume ya Uchaguzi haikuandaa uchaguzi huru na haki. Ifeanyi Okowa ni kutoka chama cha Atiku ABubakar cha PDP.

“Tunataka tume ya uchaguzi kusimamia haki na kufuta uchaguzi huu na kuaanza zoezi la uchaguzi mpya utakao kuwa huru na wa haki.”ameeleza Ifeanyi Okowa ni kutoka chama cha Atiku ABubakar cha PDP.

00:26

Ifeanyi Okowa mwakilishi wa chama cha Atiku Abubakar cha PDP

Wapinzani wanatarajiwa kwenda Mahakamani kupinga ushindi wa Tinubu, wakati huu rais huyo mteule anayetarajiwa kumrithi Muhammadu Buhari, akiwa na kazi kubwa ya kuliunganisha taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika lililogawanyika kisiasa.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.