Pata taarifa kuu

Bola Tinubu ni nani

NAIROBI – Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 70 na gavana wa zamani wa Jimbo la Lagos, kati ya mwaka 1999 hadi 2007, kwa kushinda uchaguzi huu, anatimiza ndoto yake ya miaka mingi ya kutaka kuwa rais wa nchi hiyo.

Rais anayeondoka wa Nigeria Muhammadu Buhari akiwa na rais mteule nchini humo  Bola Ahmed Tinubu
Rais anayeondoka wa Nigeria Muhammadu Buhari akiwa na rais mteule nchini humo Bola Ahmed Tinubu © Nigeria Presidency
Matangazo ya kibiashara

Kabla ya kuwa Gavana, alikuwa mwanaharakati wa kisiasa kwa kipindi kirefu na hata kukimbia nchi wakati wa utawala wa kijeshi chini ya Dikteta Sani Abacha.

Wafuasi wake wanamfahamu kwa jina la "Jagaban", kutokana na umahiri wake wa kisiasa na mchango wake wa kusaidia chama chake cha APC kuingia madarakani mwaka 2015 na kumaliza uongozi wa miaka 16 wa chama cha PDP.

Tinubu ni Mwislamu, alizaliwa katika Kabila la Yoruba, linalopatikana Kusini Magharibi mwa Nigeria.

Alisomea uhasibu nchini Marekani na kuajiriwa nchini humo, katika kampuni mbalimbali na aliwahi kuwa Mwekahazina katika kampuni ya mafuta ya ExxonMobil.

Anaelezwa pia kuwa tajiri mkubwa kutokana nabiashara zake katika sekta ya usafiri wa angaa, vyombo vya Habari, makaazi ya watu na hoteli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.