Pata taarifa kuu

Virusi vya Marburg nchini Equatorial Guinea: Vifo 9 vyathibitishwa

Ripoti ya awali ya mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Marburg ambao umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya miezi miwili nchini Equatorial Guinea inabaini kuwa watu 9 wamethibitishwa kuambukizwa vifo hivyo, Wizara ya Afya imesema leo Alhamisi.

Virusi vya Marburg viligunduliwa kwa mara ya pili Afrika Magharibi nchini Ghana.
Virusi vya Marburg viligunduliwa kwa mara ya pili Afrika Magharibi nchini Ghana. © CDC/ Dr. Frederick Murphy
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano, Shirika la Afya Duniani (WHO) liliitaka Equatorial Guinea kuripoti visa vya virusi vya Marburg kwa sababu ya hofu ya kuenea kwa maambukizi kuliko ilivyotangazwa. Mnamo Machi 23, WHO ilitaja vifo saba vilivyothibitishwa na ikatangaza kuwa inafahamu wagonjwa 20 "pengine" walioambukizwa homa hii ya hemorrhagic, ambao wote walifariki.

Kufikia Machi 28, "vifo tisa" "vimethibitishwa na maabara" tangu kuanza kwa janga la virusi vya binamu vinavyofanana na Ebola na kuua kama ugonjwa huo. "Kumekuwa na wagonjwa kumi na tatu walioambukizwa ugonjwa huo tangu kuzuka kwa janga hili, ikijumuisha wawili waliolazwa hospitalini na dalili zisizo kali, mgonjwa mmoja aliyepona na jumla ya watu 825 waliotangamana waliripotiwa," Wizara ya Afya imesema kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Shirika la Umoja wa Mataifa lilishtushwa na uwezekano wa "janga kubwa", ambalo linaweza kuathiri Gabon na Cameroon hasa, majirani wa taifa hili la Afrika ya Kati. Kesi kadha zilirikodiwa nje ya mkoa wa Kié-Ntem na kusababisha vifo vya kwanza vilivyojulikana mnamo Januari 7, hadi kufikia Bata, mji mkuu wa kiuchumi wa nchi.

WHO ilikuwa imetangaza kutumwa kwa "wataalam wengine" na kuongeza kuwa "pia inasaidia Gabon na Cameroon kuimarisha utayari na kukabiliana na janga hilo". Tanzania pia ilitangaza siku 9 zilizopita kuzuka kwa mlipuko wa Marburg, na vifo vya watu watano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.