Pata taarifa kuu

7 wafariki kutokana na virusi vya Marburg nchini E.Guinea

Watu 7 wamethibitishwa kufariki nchini Equatorial Guinea kutokana na virusi vya Marburg, huku maofisa wa afya wakisema wanachunguza ikiwa vifo vya watu wengine 20 vilitokana na ugonjwa huo, imesema taarifa ya shirika la afya duniani, WHO.

Nembo ya shirika la afya duniani WHO
Nembo ya shirika la afya duniani WHO REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko wa virusi hivi, ambavyo ni hatati kama ilivyo kwa virusi vya Ebola, kwa sasa vimeenea hadi kwenye jimbo la Kie-Ntem, ambako mgonjwa wa kwanza alifariki mwezi Januari mwaka huu.

Kwa mujibu wa Serikali kupitia wizara ya afya, ugonjwa huo umefika hata katika mji wa Bata, mji mkuu wa kibiashara wa taifa hilo.

Mkurugenzi wa shirika la afya duniani, WHO kanda ya Afrika, Dr Matshidiso Moeti, amesema mlipuko wa virusi vya Marburg, ni ishara tosha kwamba nchi zinatakiwa kuongeza kasi ya kudhibiti maambukizo zaidi, ili kuepusha ugonjwa huo kuenea kwenye maeneo mengi.

Moeti kwenye taarifa yake amesema kuwa "tangu kuripotiwa kwa ugonjwa huu, kumekuwa na jumla ya wagonjwa 9 waliothibitishwa na vipimo vya maabara na 20 wengine wakihofiwa kuwa walifariki kutokana na virusi hivi."

WHO inasema kati ya wagonjwa 9 waliothibitishwa kuwa na maambukizo, 7 wamefariki na mwingine anaendelea kupatiwa matibabu.

Mlipuko wa virusi vya Marburg, umeripotiwa pia kwenye nchi ya Tanzania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.