Pata taarifa kuu

Umoja wa Mataifa: Ukame nchini Somalia unaweza kuua watu 135 kwa siku

Ukame uliorekodiwa katika Pembe ya Afrika unaweza kusababisha vifo vya watu 135 kwa siku kati ya mwezi Januari na Juni nchini Somalia, inasema Wizara ya Afya ya Somalia, Shirika la Afya Duniani na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ​​katika utafiti uliochapishwa Jumatatu.

Punda akisubiri kubeba tanki la maji wakati wa utoaji wa maji unaoendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la Save the Children huko Kubdisha mnamo Septemba 1, 2022.
Punda akisubiri kubeba tanki la maji wakati wa utoaji wa maji unaoendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la Save the Children huko Kubdisha mnamo Septemba 1, 2022. AFP - YASUYOSHI CHIBA
Matangazo ya kibiashara

WHO ilionya hapo awali kwamba karibu watu 100,000 nchini Somalia wanakabiliwa na viwango vya janga la njaa kutokana na ukame mbaya zaidi kuwahi kukumba eneo hilo katika kipindi cha miaka 40.

Kulingana na utafiti huo uliotolewa Jumatatu, kati ya watu 18,100 na 34,200 wanaweza kufa kutokana na matokeo ya ukame nchini Somalia katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu. Hali mbaya ya hewa iliweza kusababisha "vifo vingine" 43,000 mwaka jana ikilinganishwa na ukame wa 2017, unaongeza utafiti ambao unabainisha kuwa nusu ya waathirika ni watoto walio na umri ulio chini ya miaka mitano.

Hati hii imeagizwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ​​​​na WHO na imetolewa na London School of Hygiene and Tropical Medicine na Imperial College ya London.

"Tuko katika mbio dhidi ya wakati ili kuzuia vifo na kuokoa maisha," amesema Mamunur Rahman Malik, Mwakilishi wa WHO nchini Somalia. "Gharama ya kutochukua hatua kwetu itamaanisha vifo vya watoto, wanawake na watu wengine walio katika mazingira magumu."

Misimu mitano mfululizo ya mvua iliyoambatana na uhaba mkubwa wa maji katika maeneo ya Kenya, Ethiopia na Somalia imeua mamilioni ya mifugo, kuharibu mazao na kuwalazimu zaidi ya watu milioni moja kuondoka makwao kwa kwenda kutafuta chakula na maji.

Wataalamu wa Tabia nchi wanatarajia msimu wa sita wa mvua pia kukosa maji, na hivyo kuongeza hofu ya janga la kibinadamu ambalo halijawahi kutokea katika ukanda huo, hasa nchini Somalia. Nchi hii tayari ilikumbwa na baa la njaa mwaka 2011 ambalo liliua watu 260,000, zaidi ya nusu yao wakiwa watoto walio chini ya umri wa miaka sita, kwa sababu jumuiya ya kimataifa haikuchukua hatua za haraka vya kutosha, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Mwaka 2017, zaidi ya watu milioni sita nchini Somalia, zaidi ya nusu yao wakiwa watoto, walihitaji msaada kutokana na ukame wa muda mrefu katika Afrika Mashariki. Lakini hatua za mapema za kibinadamu ziliepusha njaa mwaka huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.