Pata taarifa kuu

Papa Francis atoa wito wa kutosahau Somalia kwa majanga inayopitia

Mwishoni mwa sala ya Malaika wa Bwana (Angelus) Jumapili tarehe 14 Agosti katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kujitokeza kuelekea Pembe ya Afrika. Eneo hili limeathiriwa na ukame na njaa kali.

Papa Francis wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili Agosti 14, 2022.
Papa Francis wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili Agosti 14, 2022. © Vatican Media/­Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na ukame ambao unalikabili eneo la Pembe ya Afrika ambalo limekumbwa kwa miezi kadhaa, Papa Francis hakuficha wasiwasi wake kuhusu hali ya kibinadamu inayozidi kuwa mbaya kila siku: “Ningependa kuangazia mzozo mbaya wa kibinadamu unaoikumba Somalia. na sehemu za nchi jirani. Idadi ya watu wa eneo hili, ambao tayari wanaishi katika mazingira hatarishi, sasa wako katika hatari ya kufa kutokana na ukame. "

Lakini vita vya Ukraine na athari hizi zote kwa bahati mbaya zinapotosha hisia za jumuiya ya kimataifa, amelaumu Papa Francis, ambaye alitayarisha vipaumbele vya haraka kulingana na kiongozi huyu wa kanisa Katoliki duniani kwa Somalia: vita dhidi ya njaa, afya na elimu.

Vatican haina mwakilishi wa kidiplomasia nchini Somalia, lakini mjumbe wa kitume pekee, aliyeko Addis Ababa. Wiki iliyopita, alikuwa Mogadishu ambako alikutana na mjumbe maalum wa serikali ya Somalia kuhusu dharura za kibinadamu, Abdurahman Abdishakur. Kanisa Katoliki linajikusanya kusaidia watu walioathirika zaidi, kupitia mtandao wake wa Caritas Internationalis.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.