Pata taarifa kuu
SOMALIA-UKAME

Refugee Council yaonya kuhusu hali ya kibinadamu kuendelea kuzorota Somalia

Shirika la kutoa misaada ya kibinadamu la Norway Refugee Council la mjini Mogadishu nchini Somalia limeonya kuwa huenda watu kadhaa wakapoteza maisha huku wengine zaidi ya milioni 1 wakalazimika kuhama makwao kutokana na hali ya ukame kuendelea kuwa mbaya nchini Somalia.

Takriban watu milioni 3.2 idadi ambayo ni sawa na theluthi moja ya watu nchini humo wameathirika na ukame hali ambayo inawaweka katika hatari ya kukumbwa na njaa, utapia mlo na kupanda kwa bei za bidhaa pamoja na kupoteza mimiea na mifugo yao.
Takriban watu milioni 3.2 idadi ambayo ni sawa na theluthi moja ya watu nchini humo wameathirika na ukame hali ambayo inawaweka katika hatari ya kukumbwa na njaa, utapia mlo na kupanda kwa bei za bidhaa pamoja na kupoteza mimiea na mifugo yao. Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na shirika hilo la misaada, kwa sasa raia wa Somalia wapatao laki 2 na elfu 45 wamelazimika kuhama makwao kutokana na ukame, idadi hiyo ikikadiriwa kuongezeka hadi milioni 1.4 mwaka huu wa 2022 kutokana na hali hiyo kuendelea kuwa mbaya zaidi katika maeneo kadhaa nchini humo.

Takriban watu milioni 3.2 idadi ambayo ni sawa na theluthi moja ya watu nchini humo wameathirika na ukame hali ambayo inawaweka katika hatari ya kukumbwa na njaa, utapia mlo na kupanda kwa bei za bidhaa pamoja na kupoteza mimiea na mifugo yao.

Aidha NRC inasema kuwa wafanyakazi wake wameripoti ongezeko la vifo vinavyohusishwa na ukame, watoto wanaokumbwa na utapiamlo na watu  kutafuta misaada.

Mkurugenzi wa  shirika hilo la misaada nchini Somalia, Mohammed Abdi ametoa wito kwa nchi wafadhili kuchanga fedha zitakazosaidia kuokoa maisha kwa mamilioni ya watu walioathirika na ukame.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.