Pata taarifa kuu

Nyuklia: Tani 2.5 za uranium zatoweka katika eneomoja nchini Libya, kulingana na IAEA

Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) limeripoti kutoweka kwa takriban tani 2.5 za uranium asilia katika eneo moja nchini Libya, bila kutoa maelezo zaidi ya eneo ambalo nyuklia hiyo ilikuwepo.

Yellow cake (keki ya manjano) ni hatua ya kati katika mchakato wa kutengeneza mafuta ya nyuklia kutoka kwa madini ya uranium.
Yellow cake (keki ya manjano) ni hatua ya kati katika mchakato wa kutengeneza mafuta ya nyuklia kutoka kwa madini ya uranium. © Energy Fuels Inc./Flickr Nuclear Regulatory Commission/CC BY 2.0
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa ziara yao siku ya Jumanne, wakaguzi wa Umoja wa Mataifa "waligundua kuwa makontena kumi yenye takriban tani 2.5 za uranium asilia katika mfumo wa makinikia ya uranium ("yellow cake") hayakuwepo pale yalipotangazwa na mamlaka," mkurugenzi mkuu Rafael Grossi ameandika katika ripoti kwa nchi wanachama.

IAEA inabainisha kuwa itafanya uthibitishaji wa "ziada" ili "kufafanua mazingira ya kutoweka kwa nyenzo hii ya nyuklia na eneo ambako inapatikana kwa sasa". Hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu eneo kunakopatikana nyuklia hiyo kwa sasa.

Libya iliachan na mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia mwaka 2003 chini ya uangalizi wa kiongozi wa zamani Muammar Gaddafi.

Tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi mnamo mwaka 2011 baada ya miaka 42 ya udikteta, nchi hiyo imezama katika mzozo mkubwa wa kisiasa, huku kukiripotiwa serikali mbili hasimu zinazopingana kutoka Mashariki na Magharibi, maelfu ya wanamgambo, mamluki waliotawanyika kote nchini, bila kusahau uingiliaji wa nchi za kigeni.

Serikali mbili zinagombea madaraka: moja yenye makao yake mjini Tripoli (magharibi) na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa, nyingine ikiungwa mkono na mbabe wa kivita kutoka mashariki mwa Libya, Marshal Khalifa Haftar.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.