Pata taarifa kuu
UALAMA-ULINZI

Wakopti sita wa Misri watekwa nyara nchini Libya

Wakristo sita wa Kanisa la Kikoptiki nchini Misri wametekwa nyara na wanazuiliwa ili dhidi ya fidia katika nchi jirani ya Libya, mbunge na vyombo vya habari vilisema siku ya Alhamisi.

Waliotekwa nyara ni "wafanyakazi wa kawaida waliokwenda Libya kujaribu kutafuta kazi ya ujenzi na walitekwa nyara" walipokuwa wakisafiri kwa barabara karibu na mji wa Sabratha magharibi mwa Libya
Waliotekwa nyara ni "wafanyakazi wa kawaida waliokwenda Libya kujaribu kutafuta kazi ya ujenzi na walitekwa nyara" walipokuwa wakisafiri kwa barabara karibu na mji wa Sabratha magharibi mwa Libya REUTERS/Mohamed Abd El Ghany
Matangazo ya kibiashara

"Magenge ya wahalifu nchini Libya yaliwateka nyara Wakoti sita nchini Misri takriban wiki moja iliyopita na wanadai fidia kubwa ili kuwaachilia," Mbunge Mostafa Bakry ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Anasema waliotekwa nyara ni "wafanyakazi wa kawaida waliokwenda Libya kujaribu kutafuta kazi ya ujenzi na walitekwa nyara" walipokuwa wakisafiri kwa barabara karibu na mji wa Sabratha magharibi mwa Libya.

Vyombo vya habari vilivyo karibu na Kanisa la Coptic vilmeongeza kuwa watekaji nyara wanadai fidia ya dola 30,000 kwa kila mateka. Wamisri wengi wanaishi Libya, ambako wamepata kazi katika nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.