Pata taarifa kuu
MAENDELEO-UCHUMI

Maendeleo ya Afrika yatatizwa na ukosefu wa usalama na kuzorota kwa demokrasia

Kusonga mbele katika maendeleo ya binadamu na kiuchumi barani Afrika yanarudishwa nyuma na "kushuka kwa demokrasia" na "kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama ", kulingana na ripoti ya Wakfu wa Mo Ibrahim iliyotolewa Jumatano ambayo inatathmini utawala katika bara hilo.

Mfanyabiashara wa Sudan aliyepata uraia wa Uingereza, Mo Ibrahim (kwenye picha), aliunda taasisi yake mwaka 2006, ambayo makao yake makuu yako London na dhamira yake ni kukuza utawala bora katika bara la Afrika.
Mfanyabiashara wa Sudan aliyepata uraia wa Uingereza, Mo Ibrahim (kwenye picha), aliunda taasisi yake mwaka 2006, ambayo makao yake makuu yako London na dhamira yake ni kukuza utawala bora katika bara la Afrika. Mo Ibram Foundation
Matangazo ya kibiashara

"Hata kama kiwango cha wastani kilichofikiwa na utawala wa jumla katika bara la Afrika ni bora zaidi katika mwaka 2021 kuliko 2012", "kiwangu hiki kimeshika tangu mwaka 2019", inabainisha ripoti hiyo. "Sehemu nyingi ya bara hili haziko salama na hazina demokrasia hata kidogo mnamo mwaka 2021 kama ilivyokuwa mnamo mwaka 2012", inaendelea ripoti hiyo ambayo inasisitiza kwamba janga la Uviko-19 "limechochea hali hii ya wasiwasi".

Mauritius, Ushelisheli, Tunisia, Cape Verde na Botswana ndizo nchi zinazotawaliwa vyema, huku Sudan Kusini, Somalia na Eritrea zikishika nafasi ya chini.

Fahirisi ya Ibrahim ya Utawala wa Afrika (IIAG) imejikita katika zaidi ya viashirio 80 vilivyoainishwa katika makundi madogo manne: "usalama na utawala wa sheria", "ushiriki, haki na ushirikishwaji", "maendeleo ya binadamu" na "misingi ya fursa za kiuchumi" .

"Mwaka 2021, karibu asilimia 70 ya wakazi wa bara hili waliishi katika nchi ambayo hali ya usalama na utawala wa sheria vimezorota tangu 2012," unalaumu utafiti huo, ambao pia unabainisha kupungua kwa kasi kwa uhuru wa kutembea.

Hata hivyo, ripoti hiyo inabainisha kuwa zaidi ya 90% ya wakazi wa bara hilo wanaishi katika nchi ambayo kiwango cha maendeleo ya binadamu - ambacho kinazingatia upatikanaji wa afya, elimu, ulinzi wa kijamii na mazingira endelevu - ni cha juu.

Maendeleo ya Gambia

Katika ripoti hiyo, nchi tano zilizofanya vyema katika masuala ya utawala, kwa kuzingatia viashiria vyote, ni Mauritius, ikifuatiwa na Ushelisheli, Tunisia, Cape Verde na Botswana. Sudan Kusini ni ya mwisho nyuma ya Somalia na Eritrea. Gambia ndiyo nchi ambayo utawala wake umepata maendeleo zaidi tangu 2012, wakati badala yake ni nchi ya Libya ambayo imeshuka zaidi katika masuala yote hayo.

Ripoti hiyo pia inaangazia "muongo wa wasiwasi wa mapinduzi ya mara kwa mara katika ukanda Sahel", ikihesabu kuwa kati ya mapinduzi 29 duniani kati ya 2012 na 2021, 23 yalifanyika Afrika na hasa katika ukanda wa Sahel.

Mali na Burkina Faso, ambazo zinakabiliwa na ghasia kutoka kwa makundi ya kijihadi katika ardhi zao na ambazo zote zinatawaliwa na majeshi, zinaona viashiria vyao vya usalama vinazorota kwa kasi, katika ripoti hiyo.

Mfanyabiashara wa Sudan aliyepata uraia wa Uingereza Mo Ibrahim, aliunda taasisi yake mwaka 2006, ambayo makao yake makuu yako London na dhamira yake ni kukuza utawala bora katika bara la Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.