Pata taarifa kuu
MO IBRAHIMU-UINGEREZA-UONGOZI BORA

Tuzo ya Mo Ibrahim: Hakuna mshindi mwaka 2016

Wakfu wa Mfanyibiashara tajiri Mo Ibrahim umetangaza kuwa hakuna mshindi aliyepatikana kushinda tuzo ya kila mwaka ya Dola za Marekani Milioni 5 kwa mwaka uliopita wa 2016. 

Rais wa zamani wa Msumbiji Joaquim Chissano, mmoja wa marais wa zamani kutoka Afrika waliofanikiwa kutunukiwa tuzo ya Mo Ibrahim.
Rais wa zamani wa Msumbiji Joaquim Chissano, mmoja wa marais wa zamani kutoka Afrika waliofanikiwa kutunukiwa tuzo ya Mo Ibrahim. Liliana Henriques/RFI
Matangazo ya kibiashara

Tuzo yenye thamani ya Dola milioni 5, inatolewa kila mwaka kwa rais wa chi ya Afrika aliyeboresha usalama, afya, elimu, maendeleo ya kiuchumi na haki za kisiasa katika nchi yake, na kukabidhi madaraka kwa misingi ya kidemokrasia kwa mrithi wake.

Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa mshindi wa tuzo hii kutopatikana.

Wakfu wa Mo Ibrahim umetangaza Jumanne wiki hii kwamba hajapatikana mgombea ambaye amekamilisha sifa zote zinazohitajika mwaka 2016, kwa mara ya sita katika miaka kumi.

Shirika la Mo Ibrahim Foundation, ambapo makao yake makuu yanapatikana mjini London, bado halijampata mshindi mwaka 2009, 2010, 2012, 2013 na 2015.

Mo Ibrahim, mwenye umri wa 70, ni raia wa Uingereza mwenye asili ya Sudan, na ni bilionea aliyewekeza (zaidi ya Dola bilioni 2) katika sekta ya mawasiliano (simu za mkononi0.

Alianzisha shirika lake mjini London mwaka 2006.

Marais wa zamani wanee pekee kutoka Afrika ndi wameshapata tuzo hilo tangu mwaka 2007.

Kwa mara ya mwisho tuzo ya Mo Ibrahim ilipewa rais wa zamani wa Namibia Hifikepunye Pohamba, mwaka 2014.

Mwaka 2011 tuzo ya Mo Ibrahim ilikabidhiwa rais wa zamani wa Cape Verde Pedro Verona Pires.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela,mwanaharakati wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, alishinda tuzo hiyo mwaka 2007.

Washindi wa tuzo ya Mo Ibrahim hupokea Dola milioni 5, zinazolipwa kwa miaka 10, na kila mwaka hupewa posho ya Dola 200,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.