Pata taarifa kuu

Takriban wahamiaji 73 'wanadaiwa kufariki' kwenye pwani ya Libya

Takriban wahamiaji 73 hawajulikani waliko na inadhaniwa kuwa wamefariki kufuatia ajali ya boti kwenye pwani ya Libya siku ya Jumanne, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema katika taarifa yake leo Jumatano.

Mkasa huu wa hivi punde unafanya idadi ya vifo katika eneo la kati la Mediterania kufikia zaidi ya 130 tangu kuanza kwa mwaka wa 2023, kulingana na IOM.
Mkasa huu wa hivi punde unafanya idadi ya vifo katika eneo la kati la Mediterania kufikia zaidi ya 130 tangu kuanza kwa mwaka wa 2023, kulingana na IOM. REUTERS/Yannis Behrakis/File Photo
Matangazo ya kibiashara

"Manusura saba, ambao walirejea katika pwani ya Libya katika mazingira magumu, kwa sasa wamelazwa hospitalini," IOM imesema, na kuongeza kuwa hadi sasa maiti 11 zimepatikana na shirika la Hilali Nyekundu la Libya na polisi wa eneo hilo. Boti hilo lililozama lilikuwa limebeba takriban watu 80 kwa jumla na lilikuwa njiani kuelekea Ulaya, shirika la Umoja wa Mataifa limeongeza.

Mkasa huu wa hivi punde unaleta idadi ya vifo katika eneo la kati la Mediterania - mojawapo ya njia zinazopendelewa kwa wahamiaji wanaojaribu kufika katika bara la Ulaya - hadi vifo zaidi ya 130 tangu kuanza kwa mwaka 2023, kulingana na sensa iliyofanywa na IOM. Mnamo 2022, zaidi ya vifo 1,450 vilirekodiwa na IOM.

Mediterania ya kati inasalia kuwa kivuko cha wahamaji hatari zaidi duniani, kinachosababisha idadi kubwa zaidi ya vifo kila mwaka, linakumbusha shirika hilo la Umoja wa Mataifa, ambalo linaona hali hiyo "isiyovumilika." "Hatua za kweli za Mataifa ni muhimu kuongeza uwezo wa utafutaji na uokoaji , kuweka mifumo iliyo wazi na salama pamoja na njia salama na za kawaida za uhamiaji ili kupunguza safari hatari.

Mapema mwezi Januari, mashirika kadhaa ya kimataifa yasiyo ya kiserikali yanayohusika na shughuli za uokoaji wa wahamiaji katika Bahari ya Mediterania yalishutumu nia ya serikali ya mrengo wa kulia ya Italia "kuzuia msaada kwa watu walio katika dhiki". Yalinyooshea kidole athari za agizo la kulazimisha meli kwenda "bila kuchelewa" kwenye bandari ya Italia baada ya kila zoezi la uokoaji na mgawo wa kawaida wa bandari za mbali, kupunguza uwezo wa usaidizi.

Mstari wa mbele, Italia kwa miaka mingi imekuwa mojawapo ya lango kuu la uhamiaji kwa njia ya bahari kutoka Afrika hadi Ulaya ikiwa na rekodi ya watu 180,000 waliofika mwaka 2016. Roma inatumai hasa kupata ugawaji upya wa wahamiaji wanaowasili kwenye ardhi yake, lakini wazo hili linakabiliwa na yupinzani mkali kutoka kwa nchi nyingi za Umoja wa Ulaya, EU.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.