Pata taarifa kuu

Libya-Italia: ya ENI na NOC zasaini makubaliano ya 'kihistoria' katika sekta ya gesi

Ni mkataba muhimu ambao ulitiwa saini Jumamosi asubuhi Januari 28 huko Tripoli: Kundi la ENI litawekeza dola bilioni 8 katika maendeleo ya maeneo ya gesi ya pwani kaskazini mwa Libya. Hatimaye, mita za ujazo milioni 850 za gesi kwa siku zitazalishwa. Kwa hivyo Italia inalenga kuwa kitovu kipya cha nishati kati ya Afrika na Ulaya.

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Tripoli, Libya, Januari 28, 2023.
Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Tripoli, Libya, Januari 28, 2023. REUTERS - HAZEM AHMED
Matangazo ya kibiashara

Uthibitisho wa umuhimu wa mkataba huu: mkuu wa serikali ya Italia Georgia Meloni alifunga safari hadi Tripoli Jumamosi hii. Ziara ya hali ya juu, ya kwanza ya aina hii kwa Italia tangu ziara ya Mario Draghi mnamo mwezi Aprili 2021.

Wakati wa utiaji saini, mkuu wa kampuni ya kitaifa ya hydrocarbon ya Libya imetangaza kuwa makubaliano haya ya miaka 25 ya gesi yalikuwa uwekezaji muhimu zaidi katika sekta ya nishati ya Libya kwa robo ya karne.

Ushirikiano ulioelezewa kama "wa kihistoria" na Claudio Descalzi, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la ENI, ambalo litawezesha "uwekezaji mkubwa" katika sekta ya nishati, "uundaji wa ajira" nchini Libya na uimarishaji wa nafasi ya ENI ambayo tayari ni "chombo kinachoongoza." " kwa 80% ya uzalishaji wa gesi ya Libya.

Muhimu kiuchumi, lakini pia kijiografia. Hakika, Ulaya tangu kuzuka vita nchini Ukraine inataka kuchanganya uagizaji wake.

Mtafiti Kader Abderrahim, mtaalamu wa Libya, pia anakumbusha kwamba mamlaka ya Italia walikuwa Algiers wiki iliyopita kutia saini mikataba mikubwa ya gesi na kwamba ziara kama hiyo inatarajiwa hata Misri ambayo, kulingana na Kader Abderrahim, "ina tabaka muhimu za gesi katika Mediterania" .

"Kwa hivyo, ninaamini kwamba kuna dhamira kwa upande wa Italia kuwekeza katika uwanja mpya ambao labda pia unaleta siasa mpya za nishati wakati wa vita hivi nchini Ukraine ambavyo vinabadilisha taswira. Tunaona kwamba mkakati wa Italia ni kuepuka kuwa tegemezi kwa mshirika mmoja na wakati huo huo hii inaipa uhalali fulani wa kuwekeza tena katika nafasi ya kisiasa ya kijiografia ambayo ilikuwa imepuuzwa kwa miongo ya hivi karibuni", mtafiti Kader Abderrahim ameiambia RFI.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.