Pata taarifa kuu
LIBYA

Ufaransa, Italia na Ujerumani zataka mamluki kuondoka Libya

Baada ya wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano, na Misri siku ya Alhamisi, mawaziri watatu wa Ufaransa, Italia na Ujerumani pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Libya, katika mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari huko Tripoli, wametoa wito wa kuondoka haraka kwa mamluki nchini Libya.

Mawaziri wa Italia, Ujerumani na Ufaransa wazuri Tripoli Alhamisi, Machi 25, 2021.
Mawaziri wa Italia, Ujerumani na Ufaransa wazuri Tripoli Alhamisi, Machi 25, 2021. © Hazem Ahmed/AP
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wao wamebaini kwamba kuondoka kwa mamluki hao nchini Libya ni moja wapo ya njia ya kurejesha utulivu nchini Libya.

"Tunatoa wito kwa mamluki wote nchini Libya kuondoka mara moja nchini humo" Waziri wa Mambo ya nje wa Libya Najla al-Mangoush alitangaza siku ya Alhamisi wakati wa mkutano na waandishi wa habari pamoja na wenzake watatu kutoka Ulaya ambao wako ziarani mjini Tripoli, siku kumi tu baada ya serikali mpya ya umoja kuchukua madaraka.

Ziara hii ya kushtukiza ya mawaziri wa Ufaransa, Italia na Ujerumani nchini Libya ni dhahiri inakusudiwa kuiunga mkono serikali mpya ya umoja. "Kuondoka kwa mamluki wa kigeni ni muhimu kwa serikali ya Libya kutetea uhuru wake," amesema Jean-Yves Le Drian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.