Pata taarifa kuu
USALAMA-SIASA

Bunge la Libya lapinga ripoti ya mjumbe wa Umoja wa Mataifa

Bunge la Libya limepinga ripoti ya mjumbe wa Umoja wa Mataifa, inayoeleza kushindwa kwake kuandaa mfumo wa kisheria wa uchaguzi na kutangaza mpango mpya wa kuwezesha kufanyika kwa mfumo huo.

Libya imekuwa katika machafuko tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Libya imekuwa katika machafuko tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mjumbe huyo, Abdoulaye Bathily, raia wa Senegal, alitangaza Jumatatu kabla ya Baraza la Usalama kuzindua "mpango unaolenga kuwezesha kuandaa na kufanya uchaguzi wa urais na wa wabunge mwaka 2023" unaosimamiwa na "jopo la ngazi ya juu".

Alionyesha kushindwa kwa Baraza la Wawakilishi lenye makao yake mashariki mwa Libya na Baraza Kuu la Nchi (HCE), ambalo linafanya kazi kama Bunge la Seneti lenye makao yake makuu mjini Tripoli, "kukubaliana kwa misingi ya kikatiba ya uchaguzi".

Tumeshangazwa na makosa katika uwasilishaji huu juu ya kushindwa kwa Bunge na Baraza Kuu kupitisha misingi ya kikatiba ya kufanyika kwa uchaguzi", imebaini ofisi ya spika wa Bunge katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, ikishutumu ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya kuwa na 'upendeleo'.

Bunge lilipiga kura mnamo Februari 8 "marekebisho ya 13" ya Azimio la Katiba ambalo linatumika kama Katiba ya muda kwa kuiwasilisha kama mfumo wa kisheria wa kufanyika kwa uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Desemba 2021 lakini ukaahirishwa kwa muda usiojulikana kwa sababu ya tofauti zinazoendelea kati ya kambi hasimu. Marekebisho haya "yanapaswa kuidhinishwa na Baraza Kuu la Nchi, HCE", amesisitiza Bw. Bathily, wakati nakala tayari imechapishwa katika Jarida Rasmi na Bunge lenyewe.

"Marekebisho haya ya 13 ya katiba yamezua mijadala kwa wanasiasa nchini Libya na miongoni mwa raia" kwa kushindwa kusuluhisha "mizozo ya msingi kama vile vigezo vya mtu kuwai kwenye kiti cha urais,” ameongeza. Libya imekuwa katika machafuko tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Nchi inadhoofishwa na mgawanyiko kati ya Mashariki na Magharibi na kuingiliwa na wageni. Serikali mbili zinazohasimiana zinagombea madaraka, moja ikiwa mjini Tripoli na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa, nyingine huko Sirte (katikati), ikiungwa mkono na Bunge. Kutoelewana kuhusu mfumo wa kisheria wa uchaguzi kunahusiana hasa na masharti ambayo wagombea urais wanapaswa kutimiza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.