Pata taarifa kuu

Shambulizi la Lockerbie: Raia wa Libya azuiliwa na mamlaka ya Marekani

Abou Agila Mohammad Massoud amefunguliwa mashitaka na Marekani tangu 2020 kama sehemu ya uchunguzi wa shambulio hili la ndege ya PanAM kwenye eneo la Lockerbie, Scotland, Desemba 1988. Shambulio hilo lilisababisha vifo vya watu 270.

Shambulio la Lockerbie mnamo Desemba 1988 lilikuwa baya zaidi kuwahi kufanywa katika ardhi ya Uingereza.
Shambulio la Lockerbie mnamo Desemba 1988 lilikuwa baya zaidi kuwahi kufanywa katika ardhi ya Uingereza. AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Abou Agila Mohammad Massoud anashukiwa kukusanya na kupanga muda wa bomu lililoripua ndege ya PanAm Flight 103. Habari za kukamatwa na kuzuiliwa na mamlaka ya Marekani kwa afisa huyu wa zamani wa idara ya kijasusi ya Muammar Gaddafi zilitolewa kwa mara ya kwanza kupitia taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa upande wa mashtaka wa Scotland. Imethibitishwa na msemaji wa Idara ya Sheria ya Marekani. "Atafikishwa mahakamani katika Wilaya ya Columbia", mji mkuu Washington, upande wa mashitaka umesema katika barua pepe kwa shirika la habari la AFP. Hakuna tarehe iliyotangazwa. Mazingira ya kujisalimisha kwa mshukiwa kwa mamlaka ya Marekani pia hayajabainishwa.

Mlipuko huo wa Lockerbie ulilenga ndege iliyovuka Atlantiki kutoka London hadi New York. Ndege hiyo aina ya Boeing 747, ililipuka mnamo Desemba 21, 1988 kwenye kijiji hiki cha Scotland, na kuua abiria 259 na wafanyakazi na watu 11 ilipotua chini. Ni mtu mmoja tu ambaye alipatikana na hatia kwa shambulio hili: Abdelbaset Ali Mohamed al-Megrahi, raia wa Libya, ambaye alifariki mwaka 2012. Daima alikuwa amedumisha kutokuwa na hatia. 

Dola bilioni 2.7 kama fidia

Shambulio la Lockerbie ndilo baya zaidi kuwahi kufanywa katika ardhi ya Uingereza, lakini pia ni la pili kwa vifo dhidi ya Wamarekani (waliokufa 190) baada ya mashambulizi ya Septemba 11, 2001. Utawala wa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi ulikuwa umetambua rasmi wajibu wake mwaka 2003 na kulipa dola bilioni 2.7 za Marekani kama fidia kwa familia za wahasiriwa.

Uchunguzi huo ulizinduliwa tena mwaka wa 2016, wakati vyombo vya sheria vya Marekani vilipopata habari kwamba Abu Agila Mohammad Massoud alikamatwa baada ya utawala wa kidikteta kuanguka na kudaiwa kukiri katika idara za kijasusi za utawala mpya wa Libya mwaka 2012. Mwaka jana, mahakama ya Scotland ilikataa rufaa iliyowasilishwa na familia ya al-Megrahi, ikizingatiwa kuwa "hakukuwa na kosa la kimahakama". Mahakama pia ilifuta utetezi wa familia ya waliohukumiwa, ambao walibaini kwamba hati zinazohusiana na kesi hiyo, ambayo mamlaka ya Uingereza ilikataa kufichua, ingewezesha kutoa hukumu tofauti.

(Na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.