Pata taarifa kuu

Morocco yaomba IMF mkopo wa dola bilioni 5

Morocco imeomba rasmi IMF kuipa mkopo unaobadilika (LCM) wa dola bilioni 5, katika muktadha wa madeni makubwa ya nchi hiyo, taasisi hiyo imesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Nembo ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) nje ya jengo la makao makuu mjini Washington, Marekani.
Nembo ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) nje ya jengo la makao makuu mjini Washington, Marekani. REUTERS/Yuri Gripas/File Photo
Matangazo ya kibiashara

"Kwa kuzingatia nguvu ya mifumo ya sera ya kiuchumi ya Morocco na rekodi ya utendaji, Mkurugenzi Mkuu wa IMF Kristalina Georgieva ananuia kupendekeza kuidhinishwa kwa mpango wa MCL kwa Morocco," inaeleza taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa Jumatatu jioni.

Bodi ya wakurugenzi ya IMF ilikagua ombi la mamlaka ya Morocco siku ya Jumatatu na inatazamiwa kukutana tena katika wiki zijazo ili kuchukua uamuzi.

Ombi linalotarajiwa la Rabat linakuja wakati nchi hiyo ya Maghreb imetoka tu kwenye orodha ya kijivu ya nchi zinazokabiliwa na uangalizi ulioimarishwa na Kikosi Kazi cha Kifedha (GAFI), shirika la kupambana na utakatishaji fedha. Njia ya kutoka ambayo ustahiki wa Moroko kwa LCM ulitegemea.

Utaratibu huu wa ufadhili husaidia nchi kujikinga dhidi ya majanga kutoka nje kupitia upatikanaji wa haraka wa rasilimali za Mfuko, bila masharti ya nyuma, inakumbuhaa IMF. "Mamlaka ya Morocco inakusudia kuchukulia laini ya mkopo kama kifaa cha tahadhari," imesema taarifa hiyo.

"IMF iko tayari kuendelea kusaidia Morocco kukabiliana na hatari zinazotokana na hali ya dunia isiyo na uhakika," aimebaini taarifa hiyo. Katika miaka ya hivi majuzi, Morocco imetumia huduma nyingine ya mkopo, Precautionary and Liquidity Line (PLL). Nchi hii ya kifalme ni mojawapo ya nchi zenye madeni zaidi barani Afrika.

"Serikali inahitaji kuongeza deni sio tu kwenye soko la ndani ili kufanya nakisi ya bajeti lakini pia katika fedha za kigeni ili kukabiliana na nakisi mbaya katika usawa wa biashara, kwa dirham bilioni 312 (dola bilioni 31) kwa 2022, karibu 23%-24% ya Pato la Taifa,” anasema mwanauchumi Najib Akesbi.

"Njia ya kukopa kutoka nje pia ni ishara kwamba kuna ugumu wa kupata vifaa kwenye soko la ndani", anasisitiza Bw. Akesbi, ambaye pia ana wasiwasi kuhusu "kutoweka" kwa masharti ya upatikanaji, urejeshaji na gharama ya LCM.

Morocco inakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi kutokana na kupanda kwa bei ya vyakula na mafuta na ukuaji wa polepole. Mwishoni mwa Desemba, Benki Kuu ya Morocco (BAM) ilibidi kuongeza kiwango chake muhimu kwa pointi 50 za msingi, hadi 2.50%, ili kukabiliana na ongezeko kubwa la mfumuko wa bei (+6.6% mwaka 2022).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.