Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Mfalme Mohammed VI asitisha kazi za balozi wa Morocco nchini Ufaransa

Katika hali ya mvutano kati ya Rabat na Paris, ujumbe wa balozi wa Morocco nchini Ufaransa ulimalizika wiki hii, bila mrithi kuteuliwa. Ujumbe wa balozi wa Morocco nchini Ufaransa umemalizika bila mrithi kuteuliwa, katika hali ya mzozo wa kidiplomasia kati ya Rabat na Paris, vyombo vya habari vya ndani viliripoti Ijumaa.

Mwenyekiti wa kamati ya pamoja ya bunge la Morocco-EU Lahcen Haddad pia ameshutumu Ufaransa" kwa kuwa chanzo cha azimio la wabunge wa Umoja wa Ulaya.
Mwenyekiti wa kamati ya pamoja ya bunge la Morocco-EU Lahcen Haddad pia ameshutumu Ufaransa" kwa kuwa chanzo cha azimio la wabunge wa Umoja wa Ulaya. AP - Natacha Pisarenko
Matangazo ya kibiashara

"Kwa mujibu wa maagizo ya Juu ya Kifalme, imeamuliwa kusitisha kazi za Bw. Mohamed Benchaâboun kama Balozi wa Morocco katika Jamhuri ya Ufaransa, kuanzia Januari 19, 2023," imesema taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, iliyochapishwa katika Jarida la serikali la Februari 2.

Tarehe ya mwisho wa ujumbe wa balozi wa Morocco nchini Ufaransa "inakufika siku ambayo Bunge la Ulaya lilipiga kura azimio la wito kwa mamlaka ya Morocco kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari", vinaandika vyombo vya habari vya Hespress.

"Haiwezi kuwa bahati mbaya," inabainisha tovuti ya habari ya Medias 24, ambayo inaeleza "tangazo kuwa la utulivu na baridi kama vile hasira ya Morocco".

Kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari

Mnamo Januari 19, Bunge la Ulaya lilipitisha kwa idadi kubwa azimio lisilofunga likiwahimiza mamlaka ya Morocco "kuheshimu uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari" na kukomesha "unyanyasaji wa waandishi wa habari wote".

Wanasiasa wa Morocco na baadhi ya vyombo vya habari wameishutumu Ufaransa kwa "kuandaa" kampeni dhidi ya Morocco huko Brussels.

Mwenyekiti wa kamati ya pamoja ya bunge la Morocco-EU Lahcen Haddad pia ameshutumu "jimbo lenye kina kirefu la Ufaransa" kwa kuwa chanzo cha azimio la wabunge wa Umoja wa Ulaya.

Maandishi haya "hayaihusishi Ufaransa kwa njia yoyote", amejibu Christophe Lecourtier, balozi wa Ufaransa nchini Morocco.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.