Pata taarifa kuu
MSIMAMO MKALI-HAKI

Morocco yasitisha waraka wa kuruhusu kufukuzwa kwa imamu Hassan Iquioussen kutoka Ufaransa

Morocco haitakuwa tayari tena kumpokea imamu wa Morocco Hassan Iquioussen, ambaye Ufaransa inataka kumfukuza. Mhubiri huyo, aliyehusishwa na matamshi yanayochukuliwa kuwa kinyume na maadili ya Jamhuri, kwa sasa yuko mafichuni na anaweza kuwa nchini Ubelgiji.

Imam Hassan Iquioussen (kushoto) mnamo Juni 2004.
Imam Hassan Iquioussen (kushoto) mnamo Juni 2004. AFP - FRANCOIS LO PRESTI
Matangazo ya kibiashara

Mwezi mmoja uliopita, Morocco ilitoa hati ya kibalozi, hati inayoruhusu Ufaransa kumfukuza Imam Hassan Iquioussen. Lakini siku ya Alhamisi, chanzo kinachofahamu suala hilo kimeliambia shirika la habari la AFP kwamba pasi hii imesitishwa. Kusitishwa huko kunathibitishwa na hali ya "upande mmoja" kuhusu uamuzi wa kufukuzwa na ukosefu wa mashauriano.

Baraza la kitaifa la Ufaransa lilitoa idhni siku ya Jumanne kwa kufukuzwa kwa imamu huyo mwenye umri wa miaka 58, aliyezaliwa nchini Ufaransa, raia wa Morocco, ambaye chaneli yake ya Youtube inafuatiliwa na watu 178,000. Taasisi hiyo inaona kwamba mazungumzo yake dhidi ya Wayahudi na mazungumzo yake ya utaratibu juu ya hali duni ya wanawake ni vitendo vya kuchochea chuki. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa amemfanya Imam Iquioussen kuwa nembo ya mapambano dhidi ya wale anaowataja kuwa "wanaojitenga".

Gérald Darmanin amesema leo Alhamisi kwamba atakamatwa na kuwekwa katika kizuizi ikiwa atarejea Ufaransa. Kwa wakati huu, mhubiri huyo, anayeishi karibu na Valenciennes, kaskazini mwa Ufaransa, hapatikani. Anaweza kuwa nchini Ubelgiji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.