Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Hakuna mgogoro na Morocco, Paris yahakikisha

Ufaransa haiko katika mgogoro na Morocco, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imehakikisha siku ya Alhamisi, akijibu ukosoaji kutoka kwa wabunge wa Morocco na kampeni mbaya ya waandishi wa habari dhidi ya Ufaransa na vyombo vya habari vya ndani.

Catherine Colonna, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa.
Catherine Colonna, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa. REUTERS - SARAH MEYSSONNIER
Matangazo ya kibiashara

"Badala yakeake, tuko katika ushirikiano wa kipekee ambao tunanuia kuukuza", ametangaza Anne-Claire Legendre wakati wa mkutano na waandishi wa habari, akisisitiza nia ya Paris ya kuandika uhusiano huu wa nchi mbili "ndani ya miaka 10 hadi 20" ijayo.

Amekumbusha ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje Catherine Colonna mnamo mwezi Desemba. "Ilikuwa ziara nzuri sana," amesema, akisisitiza "ziara muhimu" ambayo atakayoifanya Rais Emmanuel Macron, na ambayo imepangwa kimsingi katika miezi mitatau ya kwanza mwaka huu.

Wanasiasa wa Morocco na vyombo vya habari vilivyo karibu na serikali vimeghadhabishwa tangu Bunge la Ulaya lilipopitisha kwa wingi wa kura wiki moja iliyopita azimio la wasiwasi kuhusu kuzorota kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini Morocco.

Bunge pia lilisema "lina wasiwasi mkubwa" na "madai kwamba mamlaka ya Morocco imepotosha wabunge wa Bunge la Ulaya". Nakala ya wabunge wa Umoja wa Ulaya ilipokelewa vibaya huko Rabat. Mshitakiwa mkuu: Ufaransa, nchi ya zamani ya kikoloni, ambayo inashutumiwa kwa "kuandaa" kampeni dhidi ya Morocco huko Brussels.

"Bunge linatekeleza haki zake kwa kujitegemea," alijibu msemaji wa Quai d'Orsay. "Kwa upande wake, Ufaransa inadumisha uhusiano wa urafiki wa kina na Morocco, ambayo inajadili masuala yote, ikiwa ni pamoja na yale ya haki za binadamu".

Katika hafla ya ziara ya Catherine Colonna, nchi hizo mbili zilionekana kupunguza mvutano na kujitangaza kuunga mkono uhusiano mpya. Lakini mara nyingi makala za vyombo vya habari zenye uhasama zimeongezeka katika siku za hivi karibuni, zikiripoti kuzorota zaidi kwa uhusiano wa Ufaransa na Morocco na kutilia shaka ujio ujao wa rais wa Ufaransa.

"Uzembe, makosa na kutoelewana kunaongezeka kati ya Paris na Rabat", linaandika jarida la Jeune Afrique siku ya Jumatano. "Kutokana na kile wanachokichukulia kuwa udhihirisho wa uhasama kwa upande wa Ufaransa, mamlaka ya Morocco haifichi tena ukweli kwamba kurejea katika hali ya kawaida itakuwa vigumu".

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.