Pata taarifa kuu

Morocco: Wanawake kutoka duniani kote watoa wito wa amani

Wanawake kutoka duniani kote waliokusanyika nchini Morocco siku ya Jumanne wametoawito wa kimataifa wa amani, "katika hali ya dharura", katika mkesha wa Siku ya Kimataifa ya Wanawake, shirika la habari la AFP limebainisha.

Wanawake wanatoa wito wa amani.
Wanawake wanatoa wito wa amani. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mpango huo unakuja "kutokana na nia ya kuunda mlolongo wa mshikamano kati ya wanawake duniani kote ili kuzindua wito wa amani, haki na usawa", ameliambia shirika la habari l AFP Hanna Assouline, rais "Peace Warriors", shirika la Wayahudi na wanawake wa Kiislamu lililoanzishwa nchini Ufaransa mwaka 2022.

Wanaharakati hawa, akiwemo Shirin Ebadi wa Iran, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, wanakutana Jumanne na Jumatano katika jiji la Essaouira (kusini mwa Morocco) "kujadili, kutafakari pamoja, kujifunza kutoka kwa kila mmoja na kutumia ahadi (zao)", amebaini mkurugenzi na mwanaharakati wa amaani kutoka shirika hilo.

Miongoni mwao, wanawake wa Israel na Palestina au kutoka Afghanistan, Syria, nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara au Morocco. "Mkusanyiko huu unawaleta pamoja wanawake kutoka duniani kote. Ni muhimu leo ​​kutambua nguvu zao," amesema Huda Abu Arqoub mkurugenzi wa shirika Amani Mashariki ya Kati (ALLMEP), kutoka Palestina ameliambia shiika la habari la AFP.

"Nina furaha kuwa miongoni mwa wanawake wa tamaduni na dini mbalimbali katika jiji linalojulikana kwa uvumilivu na maadili yake ya kuishi pamoja", alimkaribisha Shirin Ebadi, wakili wa Iran aliyeshinda Tuzo ya Nobel mwaka 2003. Mkutano huo utakamilika siku ya Alhamisi kwa "maandamano ya amani" hadi Bahari ya Atlantiki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.