Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Bola Tinubu ashinda uchaguzi wa urais nchini Nigeria

Bola Tinubu, gavana wa zamani wa Lagos, amepata kura milioni 8.8. Anafuatwa kwa karibu na aliyekuwa makamu wa rais Atiku Abubakar (kura milioni 6.9) na gavana wa zamani Peter Obi, aliyeshinda kura milioni 6.1 zilizopigwa.

Bola Tinubu, mgombea urais wa chama tawala cha APC, hapa Februari 25, 2023 mjini Lagos. Ametangazwa mshindi na Tume ya Uchaguzi mnamo Machi 1.
Bola Tinubu, mgombea urais wa chama tawala cha APC, hapa Februari 25, 2023 mjini Lagos. Ametangazwa mshindi na Tume ya Uchaguzi mnamo Machi 1. REUTERS - JAMES OATWAY
Matangazo ya kibiashara

Mgombea wa chama tawala nchini Nigeria, Bola Tinubu, ametangazwa leo Jumatano mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumamosi, kulingana na tangazo muhimu la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Bw. Tinubu, wa chama cha Congress of Progressives (APC), amepata kura 8,794,726, mwenyekiti wa INEC ametangaza kutoka kituo cha kitaifa cha kukusanya kura za jimbo kwa jimbo zinazotangazwa moja kwa moja kwenye televisheni.

Kwa hivyo yuko mbele ya washindani wake wawili wakuu kwa tofauti ndogo, baada ya moja ya chaguzi zenye ushindani mkubwa katika historia ya kidemokrasia ya Nigeria.

Atiku Abubakar, mgombea wa chama kikuu cha upinzani (PDP kilichotawala nchi kutoka 1999 hadi 2015) amepata kura milioni 6.9.

Anafuatwa kwa karibu na Peter Obi wa Chama cha Labour (LP), ambaye aliamsha matumaini makubwa miongoni mwa vijana, na kukusanya kura milioni 6.1.

Ili kuchaguliwa kuwa rais wa Nigeria, ni muhimu kupata angalau asilimia 25 ya kura katika angalau theluthi mbili ya majimbo 36 ya shirikisho hilo pamoja na eneo la mji mkuu Abuja.

Kabla ya kumalizika kwa hesabu hiyo, upinzani ulikuwa tayari umetoa wito wa kufutwa kwa uchaguzi, ukilaani udanganyifu 'mkubwa'.

Akiwa na umri wa miaka 70, Bola Tinubu, gavana wa zamani wa Lagos atamrithi Rais anayemaliza muda wake Muhammadu Buhari, 80, ambaye anajiuzulu baada ya mihula miwili kama inavyotakiwa na Katiba.

Ikiwa na wakazi wake milioni 216, Nigeria inapaswa kuwa nchi ya tatu yenye watu wengi zaidi duniani ifikapo 2050.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.