Pata taarifa kuu

Nigeria: Upinzani wapinga matokeo yanayotangazwa na tume ya uchaguzi

NAIROBI – Nchini Nigeria, Bola Tinubu mgombea wa urais kupitia chama tawala cha APC, anaongoza kwa kura Milioni 3. 8 mujibu wa matokeo ambayo yanaendelea kutangazwa, huku mpinzani wake wa karibu Atiku Abubakar akiwa na kura Milioni 3 na Peter Obi wa chama cha Leba, akiwa na kura Milioni 1.6.

Tume ya uchaguzi nchini Nigeria inaendelea na zoezi la kuhesabu kura za urais
Tume ya uchaguzi nchini Nigeria inaendelea na zoezi la kuhesabu kura za urais © Voice of Nigeria
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, vyama vya upinzani vikiongozwa na PDP vimedai kuwa, kuna njama ya kuiba kura na jana vilijondoa kwenye ukumbi wa kujumuisha matokeo. Dino Melaye ni Wakala wa Atiku Abubakar.

“Sisi mawakala wa vyama tumetathmini kwamba mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ana nia ya kuiba kura kwa kuhakikisha kwamba matokeo hayawekwi wazi kwenye matokeo ya tume.” ameeleza Dino Melaye ni Wakala wa Atiku Abubakar.

00:23

Dino Melaye ni Wakala wa Atiku Abubakar

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Mahmood Yakubu ameviambia vyama vya siasa vilivyo na malalamishi kuyawasiliha kwa Tume.

“Tume ina mamlaka kwa mujibu wa tume ya uchaguzi kupitia upya matokeo yote lakini hilo linaweza kufanyika baada ya zoezi hilo kukamilika.” ameeleza Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Mahmood Yakubu.

00:26

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria, Mahmood Yakubu

Matokeo zaidi yanatarajiwa kutangazwa leo, wakati huu raia wa nchi hiyo, wakimsubiri mshindi wa uchaguzi huo uliofanyika Jumamosi iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.