Pata taarifa kuu
UCHAGUZI - NIGERIA

Nigeria: INEC yaombwa kuinusuru nchi wakati upinzani ukitaka uchaguzi ufutwe

Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, ametoa wito kwa tume ya uchaguzi nchini humo kuinusuru nchi hiyo na machafuko.

Aliyekuwa rais wa Nigeria Olusegun Obasanjo
Aliyekuwa rais wa Nigeria Olusegun Obasanjo REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Obasanjo inakuja kutokana na kile anachosema ni rushwa iliyokithiri katika mchakato wa uchaguzi wa mwishoni mwa juma lililopita.

Mwenyekiti wa INEC anaweza kujifanya mjinga, kwamba hawezi kukunjua mikono na kufanya kitu, wakati anajua fika mchakato wa uchaguzi  uligubikwa na rushwa. Hebu nimwombe mwenyekiti wa INEC kama mikono yake ni safi kuiokoa  Nigeria kutokana na hatari  na maafa yanayotunyemelea. Amesema Olusegun Obasanjo.

Wito wa Olusegun unakuja wakati huu upinzani siku ya Jumanne, uliomba uchaguzi huo kufutiliwa mbali kwa madai kuwa uchgauzi huo unaonyesha katika matokeo ya awali kuwa mgombea wa chama tawala ccha APC Bola Tibunu anaongoza, yamekarabatiwa.

Mwenyekiti wa Chama cha Labour Julius Abure amewaambia waandishi wa habari pamoja na wawakilishi wa PDP kuwa uchaguzi umetatizika na wamepoteza imani na mchakato mzima.

Tunadai kwamba udanganyifu huu wa uchaguzi unapaswa kufutwa mara moja, pia tunaomba uchaguzi mpya ufanyike. Amesema Abure

Huku Rais Muhammadu Buhari akiondoka madarakani, wananchi wengi wa Nigeria walitumai kura hiyo ya Jumamosi ingefungua njia kwa kiongozi anayeweza kukabiliana na ukosefu wa usalama, kupunguza hali mbaya ya kiuchumi na kudhibiti umaskini katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.