Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi wa urais Nigeria: Tinubu aongoza, upinzani wadai wizi wa kura

Zoezi la uhesabuji wa kura baada ya uchaguzi wa urais linaanza tena leo Jumanne nchini Nigeria ambapo Bola Tinubu, mgombea wa chama tawala, anaonekana kuongoza kulingana na kura zilizohesabiwa, lakini vyama vya wagombea wawili wa upinzani vinalaani "udanganyifu" wa matokeo.

Matokeo katika majimbo mengi bado hayajatangazwa, hasa yale ya Kano (kaskazini), Kaduna (kaskazini-magharibi) na Rivers (kusini-mashariki).Nearly 90 million were eligible to vote on Saturday for a successor to President Muhammadu Buhari, with many hoping for a new leader to tackle insecurity, economic malaise and widening poverty.
Matokeo katika majimbo mengi bado hayajatangazwa, hasa yale ya Kano (kaskazini), Kaduna (kaskazini-magharibi) na Rivers (kusini-mashariki).Nearly 90 million were eligible to vote on Saturday for a successor to President Muhammadu Buhari, with many hoping for a new leader to tackle insecurity, economic malaise and widening poverty. AFP - PIUS UTOMI EKPEI
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya wapiga kura milioni 87 walipiga kura siku ya Jumamosi kumchagua miongoni mwa wagombea 18 mtu ambaye atakuwa na kazi ngumu kwa miaka minne ya kurekebisha nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika, inayolemewa na kudororoa kwa uchumi, ghasia za mara kwa mara za makundi yenye silaha na majambazi, pamoja na umaskini wa jumla unaowakabili raia.

Raia wa Nigeria walimchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari, 80, ambaye hakuwaia katika uchaguzi huo baada ya mihula miwili (kama Katiba inavyotaka), lakini pia wabunge wao na maseneta. Tume ya Uchaguzi iliahirisha Jumatatu jioni zoezi la uhesabuji wa kura. Hadi sasa ilikuwa imetangaza matokeo rasmi katika majimbo 14 kati ya 36 nchini humo na katika mji mkuu wa shirikisho Abuja.

Kwa sasa, Bola Tinubu, wa APC, chama cha rais aliyeko madarakani, anaongoza kwa zaidi ya kura milioni 3.8, dhidi ya kura milioni 3 za Atiku Abubakar, mgombea wa PDP, chama kikuu cha upinzani. Wawili hao wako mbele ya Peter Obi ambaye umaarufu wake kwa vijana wanaomwona kuwa mwadilifu na mwenye uwezo umeshangaza kila mtu: mgombea anayeungwa mkono na chama cha Labour Party (LP) hadi sasa amepata kura milioni 1.6. .

Matokeo katika majimbo mengi bado hayajatangazwa, hasa yale ya Kano (kaskazini), Kaduna (kaskazini-magharibi) na Rivers (kusini-mashariki).

Shutma za udanganyifu

Kura ya Jumamosi kwa ujumla ilifanyika vizuri, licha ya matukio machache ya usalama. Lakini kucheleweshwa kwa hesabu, na kasoro katika uhamishaji wa matokeo kielektroniki (yaliyojaribiwa kwa mara ya kwanza katika ngazi ya kitaifa) kumechochea wasiwasi na shutuma za udanganyifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.