Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Wanaigeria wasuburi kutangazwa kwa rais mpya, lakini shinikizo ni kubwa kwa INEC

Nigeria inasubiri takwimu za kwanza za uchaguzi wa urais na wa wabunge ambao wakati mwingine muda umesogezwa mbele Jumapili hii asubuhi kutokana na matatizo ya kiufundi. Matarajio na shinikizo ni kubwa kwa INEC, Tume Huru ya Uchaguzi, kuhakikisha matokeo ya uwazi na ya kuaminika.

Uchaguzi wa Jumamosi Februari 25 umegonga vichwa vya habari nchini Nigeria Jumapili hii.
Uchaguzi wa Jumamosi Februari 25 umegonga vichwa vya habari nchini Nigeria Jumapili hii. AP - Ben Curtis
Matangazo ya kibiashara

Zoezi la  kutangaza matokeo ya uchaguzi limeanza vizuri Jumapili baada ya Alaasiri huko Abuja, lakini utangazaji wa matokeo unakabiliwa na kizungumkuti na Tume ya Uchaguzi ilisimamisha kazi yake haraka sana, ikitangaza kwamba itaanza kazi yake Jumatatu kuanzia saa tano mchana.

" Lazima tulinde kura zetu " mara nyingi ilisikika wakati wa kampeni. Katika chaguzi zilizopita za urais, ilibidi kusubiri siku kadhaa baada ya uchaguzi ili kutangazwa rasmi kwa matokeo. Hata hivyo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ameahidi kwamba matokeo yatatangazwa "haraka", lakini hakutaja tarehe ya mwisho, na kuongeza uwezekano kwamba tarehe hii ya mwisho inahesabiwa kwa siku. Kuhesabu kura katika nchi hiyo yenye wakazi wengi zaidi barani Afrika huchukua muda: zaidi ya wapiga kura milioni 93 waliitwa kupiga kura siku ya Jumamosi, kura ambayo imeendelea katika baadhi ya vituo vya kupigia kura Jumapili hii.

Kumbuka kwamba ili kuchaguliwa, rais wa mpya wa shirikisho la Nigeria atalazimika kupata idadi kubwa ya kura. Lakini pia zaidi ya asilimia 25 ya kura zilizopigwa katika angalau theluthi mbili ya majimbo nchini, kwa hiyo 24 kati ya 36. Vinginevyo, Katiba inatoa nafasi ya duru ya pili kati ya wagombea wawili wenye alama bora zaidi. Hali ambayo haijawahi kutokea tangu kurejeshwa kwa raia madarakani mwaka 1999.

Wakatri huo huo mvutano umeanza kujitokeza kati ya vyama vya kisiasa viliwania katika uchaguzi huo, baadhi vinadai kura zirejelewe kuhesabiwa katika baadh ya majimbo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.