Pata taarifa kuu

Askofu mkuu wa Algiers, raia wa Ufaransa achukua uraia wa Algeria

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune siku ya Jumatatu amempa uraia wa Algeria Askofu Mkuu wa Algiers, Mfaransa Jean-Paul Vesco, aliyeteuliwa kushika wadhifa huu mnamo mwezi Desemba 2021.

Kanisa kuu la Notre Dame d'Afrique huko Algiers.
Kanisa kuu la Notre Dame d'Afrique huko Algiers. (Photo : AFP)
Matangazo ya kibiashara

Kwa sheria ya rais, "amepata uraia wa Algeria. Vesco Jean Paul alizaliwa Machi 10, 1962 huko Lyon (Ufaransa)", imesema taarifa kutoka ikulu ya rais wa Algeria.

Askofu Vesco alipewa Daraja Takatifu la Upadre kwa Kanisa la Dominika mwezi Juni 2001. Septemba 2002, aliteuliwa kushika wadhifa huo katika dayosisi ya Oran (magharibi mwa Algeria) kabla ya kuwa Vicar General of Oran mwaka 2005 hadi 2010, alipoondoka Algeria na kurejea Ufaransa.

Mnamo Desemba 2012, alirejea Algeria tena kama Askofu wa Oran kabla ya kuteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Algiers mnamo mwezi Desemba 2021 na Papa Francis. Tangazo la kukabidhiwa uraia wa Algeria kwa Askofu Vesco linakuja katika mazingira ya mvutano kati ya Ufaransa na Algeria.

Algiers ilimwita balozi wake mjini Paris mapema mwezi Februari kwa mashauriano baada ya kuwashutumu wanadiplomasia wa Ufaransa na maafisa wa usalama kwa "kumtoa kinyume cha sheria" mwanaharakati wa mwennye uraia pacha (Ufaransa na Algeria) kutoka Tunisia kumbeba Ufaransa.

Hata hivyo katika mwaka 2021, Paris na Algiers zilifufua uhusiano wao wakati wa ziara ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron huko Algiers mwezi Agosti mwaka uliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.