Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Rais wa Algeria kuzuru Ufaransa mwezi Mei kwa ziara ya kiserikali

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron walikubaliana siku ya Jumapili kupanga ziara ya serikali ya Tebboune nchini Ufaransa "kwa mwezi Mei mwaka huu", wakati wa mazungumzo ya simu, kulingana na rais wa Algeria.

Emmanuel Macron na Abdelmadjid Tebboune walitia saini Jumamosi hii, Agosti 27 mjini Algiers maridhiano kati ya nchi zao mbili, miaka 60 baada ya kumalizika kwa vita vya Algeria.
Emmanuel Macron na Abdelmadjid Tebboune walitia saini Jumamosi hii, Agosti 27 mjini Algiers maridhiano kati ya nchi zao mbili, miaka 60 baada ya kumalizika kwa vita vya Algeria. © Anis Belghoul / AP
Matangazo ya kibiashara

Marais hao wawili walijadili "maswali yanayohusiana na uhusiano wa nchi mbili na ziara ya serikali ya Rais wa Jamhuri nchini Ufaransa, na kukubaliana kuipanga kwa mwezi wa Mei," imesema ikulu ya rais katika taarifa yake.

Katika mahojiano na mwandishi wa Algeria Kamel Daoud yaliyochapishwa Januari 11 na gazeti la kila wiki la Le Point, Bw. Macron alisema anatumai kumkaribisha Bw. Tebboune nchini Ufaransa mwaka 2023 ili kuendeleza kazi ya kumbukumbu na maridhiano kati ya nchi hizo mbili.

Mwishoni mwa mwezi Desemba, Bw. Tebboune alikuwa amekaribisha "uhusiano mpya wa kuaminiana" kati ya Ufaransa na Algeria, miezi minne baada ya ziara ya Bw. Macron mjini Algiers na kutangaza ziara ya kitaifa nchini Ufaransa mwaka 2023, katika mahojiano na gazeti la kila siku la Ufaransa la Le Figaro.

Wakuu hao wawili wa nchi walizindua upya ushirikiano wa nchi hizo mbili katika tamko la pamoja lililotiwa saini kwa shangwe mwishoni mwa mwezi Agosti, na hivyo kufungua njia hasa ya kulegeza masharti ya utaratibu wa visa iliopewa Algeria, badala ya kuongeza ushirikiano kutoka kwa Algiers dhidi ya uhamiaji haramu.

Swali hilo lilitia sumu uhusiano baina ya nchi hizo mbili baada ya Paris kupunguza nusu ya idadi ya visa iliyopewa Algeria katika msimu wa joto wa 2021, ambayo haikuonekana kuwa ya haraka kwa kuwapokea raia wake waliofukuzwa kutoka Ufaransa.

Lakini kesi hiyo ilitatuliwa katikati ya mwezi wa Desemba wakati Ufaransa ilitangaza, kupitia Waziri wake wa Mambo ya Ndani Gérald Darmanin, kurejea katika hali ya kawaida katika utoaji wa visa kwa raia wa Algeria, baada ya uamuzi sawa na huo kwa Watunisia na Wamorocco.

Swali la ukumbusho kuhusu ukoloni wa Ufaransa (1830-1962) na vita vya umwagaji damu vya ukombozi (1954-1962) vilisababisha ugomvi mkubwa kati ya nchi hizo mbili katika msimu wa joto wa 2021, baada ya matamshi ya Bw. Macron ambayo alirekebisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.