Pata taarifa kuu

Paris na Algiers zasaini 'ushirikiano mpya'

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wameboresha maridhiano kati ya nchi zao mbili siku ya Jumamosi kwa kutia saini tamko ambalo "linaboresha dhamira yao ya kuweka uhusiano wao katika hali ya maendeleo yasiyoweza kutenduliwa".

Emmanuel Macron et Abdelmadjid wameboresha maridhiano kati ya nchi zao mbili siku ya Jumamosi hii, Agosti 27 mjini Algiers, miaka 60 baada ya kumalizika kwa vita vya Algeria.
Emmanuel Macron et Abdelmadjid wameboresha maridhiano kati ya nchi zao mbili siku ya Jumamosi hii, Agosti 27 mjini Algiers, miaka 60 baada ya kumalizika kwa vita vya Algeria. AP - Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

"Nzuri na yenye mafanikio". Abdelmadjid Tebboune amejawa na furaha kwa ziara ya mwenzake rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. "Ziara hii imewezesha ukaribu ambao haungewezekana bila utu wa Rais Macron", amekaribisha rais wa Algeria, ambaye alizungumza kwa Kifaransa. Kulingana na Rais Abdelmadjid Tebboune , nchi hizo mbili "zitachukuwa hatua pamoja katika nyanja nyingi nje ya Algeria na Ufaransa". "Ukaribu huu utatuezesha kwenda mbali zaidi," ameongeza.

Abdelmadjid Tebboune ametaja mkutano wa ngazi ya juu ambao umewakutanisha marais na vyombo vya usalama vya pande zote mbili, likiwemo jeshi, "kwa mara ya kwanza tangu uhuru" wa Algeria mwaka 1962, na kutangaza hatua za pamoja "kwa maslahi ya mazingira yetu ya kijiografia na kisiasa".

'Mahitaji'

Ili "kuimarisha mashauriano yao ya kisiasa", Paris na Algiers wataunda "Baraza Kuu la Ushirikiano" katika ngazi ya Wakuu wa Nchi, ili "kuimarisha, kwa moyo wa kuaminiana na kuheshimiana, majibu sahihi kwa nchi mbili, kikanda na masuala ya kimataifa", tamko hilo la pamoja la Marais hao wawili huko Algiers limebaini.

Kulingana na taarifa hiyo, "ushirikiano huu mpya wa hali ya juu" "umekuwa hitaji linaloamriwa na kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na uhakika na kuzidisha kwa mivutano ya kikanda na kimataifa". "Taarifa hiyo inatoa mfumo wa kubuni dira ya pamoja na mbinu iliyounganishwa kwa karibu ili kukabiliana na changamoto mpya za kimataifa (migogoro ya kimataifa na kikanda, mabadiliko ya hali ya hewa, uhifadhi wa viumbe hai, maendeleo ya kidijitali, afya ...)", linasema tamko hilo.

Azimio la Algiers litawezesha kuhakikisha kwamba “urafiki unaimarishwa kwa kuwa na mazungumzo ya kudumu kuhusu masuala yote. Ikiwa ni pamoja na masuala ambayo yalituzuia kusonga mbele, kwa sababu yaliendelea kujirudi, kumbukumbu kwa mfano, "amehakikisha Emmanuel Macron kwa upande wake. Swali la ukumbusho kuhusiana na ukoloni wa Ufaransa (1830-1962) lilisababisha mgogoro mkubwa kati ya nchi hizo mbili msimu uliopita. Tume ya pamoja ya wanahistoria iliamua wakati wa ziara ya wajumbe wa Ufaransa kuondoa kutokubaliana na kukabiliana na siku za nyuma "kwa ujasiri", kulingana na maneno ya Emmanuel Macron, "inaweza kukuudwa katika siku 15 hadi 20 ", ametangaza Abdelmadjid Tebboune.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.