Pata taarifa kuu

Algeria: Macron atangaza tume ya wanahistoria kutoka nchi zote mbili kuhusu kumbukumbu

Katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi nchini Algeria, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alizungumza kwa kirefu na mwenyeji wake rais wa Algeria Abdelmajid Tebboune. Mwishoni mwa mazungumzo hayo, marais hao wawili walitoa taarifa katika Ikulu ya El Mouradia na kujitahidi kuonyesha nia yao ya kuzindua upya ushirikiano kati ya Ufaransa na Algeria. Lakini kwa upande wa Emmanuel Macron, anasema ziara hii imewezesha maendeleo kwenye nyanja ya kumbukumbu.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Algeria Abdelmajid Tebboune, Agosti 25, 2022 huko Algiers.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Algeria Abdelmajid Tebboune, Agosti 25, 2022 huko Algiers. AP - Anis Belghoul
Matangazo ya kibiashara

Emmanuel Macron na Abdelmadjid Tebboune hawakuachana baada ya kupeana mkono, alipofika kwenye uwanja wa ndege wa Algiers-Houari-Boumédiène. Wote wawili walikagua wanajeshi kabla ya nyimbo za kitaifa. Marais hao wawili walifanya mazungumzo mara ya kwanza katika chumba cha mapumziko cha uwanja wa ndege, wakiwa wamezungukwa na mawaziri wao wakuu.

Emmanuel Macron kisha akaenda kwenye Ukumbusho wa Mashuja, hatua muhimu kwa ziara rasmi nchini Algeria, kabla ya kuungana na Abdelmadjid Tebboune kwenye ikulu ya rais ya El Mouradia, kwenye mmilima ya Algiers. Viongozi hao wawili walifanya mkutano wao wa kwanza wa ana kwa ana.

Ili kufunga siku hii ya kwanza ya Emmanuel Macron nchini Algeria, chakula cha jioni kiliandaliwa kwa heshima yake katika makao makuu ya Bunge. Hili lilifuatiwa na tamko la pamoja, ambapo Abdelmajid Tebboune alisifu "matokeo ya kutia moyo" ambayo yanawezesha "kuwa na matumaini". Alisisitiza juu ya azma ya nchi hizo mbili "kusonga mbele" na "kuimarisha juhudi za kuimarisha uhusiano". 

Emmanuel Macron, kwa upande wake, alitangaza kuanzishwa kwa tume ya pamoja ya wanahistoria wa Algeria na Ufaransa kuchunguza kumbukumbu za ukoloni na vita nchini Algeria. "Tuna historia ya pamoja, (...) ngumu, yenye huzuni," alisema rais wa Ufaransa ambaye alichaguliwa tena mwezi Mei mwaka jana. Yeye na Abdelmajid Tebboune "wameamua kwa pamoja" kuundwa kwa tume hii ambayo itakuwa na jukumu la "kutazama kipindi chote cha kihistoria", "tangu mwanzo wa ukoloni hadi vita vya ukombozi, bila mwiko, kwa nia (. .) ya kupata bila kizuizi chochote kumbukumbu zetu”.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.