Pata taarifa kuu

Emmanuel Macron nchini Algeria kwa ziara ambayo inalenga kuimarisha ushirikiano

Emmanuel Macron anasafri kwenda Algeria Alhamisi hii, Agosti 25 kwa ziara ya siku tatu, kwa mwaliko wa Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune. Hii ni ziara yake ya pili kama mkuu wa nchi, na ataandamana na ujumbe mkubwa wa watu takriban 90. Kwa ziara hii, rais wa Ufaransa anatarajia kugeuza ukurasa kwenye mlolongo mgumu katika uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kuonyesha mtazamo mpya katika siku zijazo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anazuru Algeria siku ya Alhamisi kwa ziara ya siku tatu, kwa mwaliko wa Rais wa Algeria Abdelmajid Tebboune. Hii ni ziara yake ya pili kama mkuu wa nchi, baada ya ziara ya kwanza mwaka wa 2017.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anazuru Algeria siku ya Alhamisi kwa ziara ya siku tatu, kwa mwaliko wa Rais wa Algeria Abdelmajid Tebboune. Hii ni ziara yake ya pili kama mkuu wa nchi, baada ya ziara ya kwanza mwaka wa 2017. © AP/Gonzalo Fuentes
Matangazo ya kibiashara

Ziara "rasmi na ya kirafiki", na sio ya kiserikali, hivi ndivyo marais hao wawili wameamua kuitaja ziara hii ya Emmanuel Macron nchini Algeria. Maneno haya yana maana na katika Ikulu ya Élysée, inatambulika kwamba hii inalingana na hatua ambayo ziara hii itaashiria katika mahusiano ya Ufaransa na Algeria, ambayo yalikuwa yamekumbwa na kizingi mkuti.

Katika swali hili, hasa: maoni ya Emmanuel Macron ambayo yaliikasirisha Algiers. Rais wa Ufaransa alikadiria mnamo 2021 kwamba serikali ya Algeria ilitumia "kodi ya kumbukumbu" na alishangazwa juu ya uwepo wa taifa la Algeria kabla ya ukoloni. Emmanuel Macron kisha alisikitishwa na jinsi maneno yake "hayakueleweka". Suala lingine lililosababisha sintofahamu kati ya nchi hizi mbili: mvutano kuhusu utoaji wa visa ambapo Paris iliamua kupunguza idadi ya kutoa visa, suala ambalo limeanza kupatiwa suluhu, kulingana na ikulu ya Élysée.

Emmanuel Macron anawasili Algiers akiwa na nia ya kufufua uhusiano uliodorora kwa mivutano kati ya nchi hizi mbili. Kwa kukaa siku tatu nchini humo na pia kwenda Oran, anataka kuonyesha umuhimu wa ziara hii na kuhutubia wananchi wote wa Algeria, na hasa vijana. Rais wa Ufaransa atakutana hasa na wafanyabiashara vijana. Lengo lililotajwa ni kuweka "msingi" wa kujenga upya uhusiano na kuzungumza juu ya hatima ya uhusiano kati ya nchi hiz mbili, na sio tu suala la kumbukumbu, hata kama rais anataka kuendelea na kazi ya kuenzi kumbukumbu, iliyoanzishwa nchini Ufaransa na ripoti ya Stora.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.