Pata taarifa kuu

Mahusiano ya kiuchumi kati ya Ufaransa na Algeria

Maridhiano, kumbukumbu, lakini pia ulinzi na usalama ni masuala nyeti ambayo yataangaziwa katika ziara ya Emmanuel Macron nchini Algeria. Lakini hatagusia suala la uchumi, wakati alitangaza Jumatano hii kwamba "uzembe" sasa umefikia kikomo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Algeria Abdelmadjid Tebboune.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Algeria Abdelmadjid Tebboune. © AP/AFP/Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Swali la kuhakikisha usambazaji wa gesi katika mazingira ya vita nchini Ukraine haliwezi kuepukwa katika mazungumzo yake na rais wa Algeria. Takriban 10% ya gesi inayotumiwa nchini Ufaransa inatoka Algeria. Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Engie ni sehemu ya safari hiyo, pamoja na Waziri wa Uchumi, Bruno Le Maire.

Hata hivyo, hakutakuwa na tangazo kubwa katika nyanja ya uchumi, wala mikataba mikubwa wala mazungumzo makubwa, tayari kulingana na vyanzo kutoka serikalini. Masuala ya nishati, madini au viwanda yanaweza kushujadiliwa katika mazungumzo ya marais ao wawili, lakini sio lengo la ziara hiyo.

Ikiwa uhusiano wa kidiplomasia umekumbwa na msukosuko katika miezi ya hivi karibuni, kiuchumi, nchi hizo mbili zinasalia kuwa washirika wakubwa. Mnamo 2020, Ufaransa ilikuwa muuzaji wa pili wa Algeria na mteja wa pili katika suala la biashara. Usafiri, magari, kilimo cha chakula, benki na bima, au hata duka la dawa, ni sekta za shughuli ambazo makampuni ya Ufaransa yanawekeza zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.