Pata taarifa kuu
ALGERIA-DIPLOMASIA

Balozi wa Algeria nchini Ufaransa arejea kazini

Balozi wa Algeria nchini Ufaransa, ambaye aliitishwa tena nyumbani mwezi Oktoba "kwa mashauriano" baada ya kauli za Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron zilizochukuliwa kuwa za kuudhi na Algiers, ataanza kazi yake Alhamisi, Januari 6, ofisi ya rais wa Algeria imetangaza Jumatano.

Sehemu ya mbele ya ubalozi wa Algeria huko Paris, mnamo Julai 2021.
Sehemu ya mbele ya ubalozi wa Algeria huko Paris, mnamo Julai 2021. AFP - JOEL SAGET
Matangazo ya kibiashara

Rais Abdelmadjid Tebboune "alimpokea Jumatano balozi wa Algeria nchini Ufaransa, Mohamed Antar-Daoud, ambaye ataanza tena majukumu yake mjini Paris kuanzia Alhamisi hii, Januari 6, 2022," ofisi ya rais imesema katika taarifa.

Algiers ilimuitisha nyumbani balozi wake Oktoba 2 kutokana na kauli zilizotolewa na rais wa Ufaransa kupitia Gazeti la Le Monde ambalo lilithibitisha kwamba Algeria, baada ya uhuru wake mwaka 1962, ilikuwa imejengwa kwa "kodi ya kumbukumbu", iliyodumishwa na "mfumo wa kisiasa na kijeshi " . Emmanuel Macron pia alihoji kuwepo kwa taifa la Algeria kabla ya enzi za ukoloni wa Ufaransa kuanzia mwaka 1830.

Algiers ilichukuwa hatua, na kupiga marufuku kuruka juu kwenye  anga yake kwa ndege za kijeshi za Ufaransa zinazohudumu katika ukanda wa Sahel, ambapo wanajeshi wa oparesheni ya kupambana na wajihadi ya Barkhane wametumwa.

Rais wa Algeria pia alionya mapema mwezi Novemba kwamba hatachukua "hatua ya kwanza" kujaribu kutuliza mivutano.

Emmanuel Macron tangu wakati huo alielezea masikitiko" yake katika utata uliyotokana na kusema "ameshikamana sana na maendeleo" ya uhusiano wa pande mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.