Pata taarifa kuu
UFARANSA-ALGERIA-DIPLOMASIA

Macron alaani mauaji ya waandamanaji wa Algeria waliokuwa wanadai uhuru 1961

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amelaani mauaji yaliyotekelezwa na polisi chini ya aliyekuwa Kamanda wa jijini la Paris Maurice Papon  dhidi ya waandamanaji wa Algeria waliokuwa wanadai uhuru wa nchi yao mwaka  Oktoba 17 1961.

Rais wa Ufaransa  Emmanuel Macron, akiweka shada la maua mwaka 16/10/2021 katika eneo ambalo waandamanaji wa Algeria waliuawa mwaka 1961 wakidai uhuru
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, akiweka shada la maua mwaka 16/10/2021 katika eneo ambalo waandamanaji wa Algeria waliuawa mwaka 1961 wakidai uhuru Rafael Yaghobzadeh POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na ndugu na wanaharakati katika maadhimisho ya miaka 60 jijini Paris, Macron ambaye amekuwa kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo kushiriki kwenye maadhimisho hayo, amesema mauaji hayo yaliyosababisha mamia ya watu hayawezi kutetewa na hayakupaswa kutokea.

Tarehe 17 mwezi Oktoba mwaka 1961, polisi kutoka  jijini Paris waliwapiga risasi na kuwauwa waandamanaji waliokuwa wanapinga ukoloni wa Ufaransa nchini Algeria.

Mpaka sasa haijafahamika ni watu wangapi walipoteza maisha kwenye maandamano hayo, lakini wanahistoria wanasema, mamia ya watu waliuawa.

Swali kubwa ambalo limekuwa likusubiriwa kwa muda huo wote na raia wa Algeria ni iwapo Ufaransa itaomba radhi kwa vitendo hivyo vya polisi wakati huu rais Macron anapolenga kuimarisha uhusiano kati ya nchi hiyo ya Afrika Kaskazini.

Wanaharakati wamekuwa wakitaka Ufaransa kuomba radhi, kinyume na matamshi ya rais wa zamani Francois Hollande, aliyekiri mwaka 2012 kuwa, raia wa Algeria waliokuwa wanaandamana kupinga ukoloni, waliuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.