Pata taarifa kuu

Oktoba 17, 1961: Emmanuel Macron alaani "uhalifu usiosamehewa kwa Jamhuri"

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Jumamosi, Oktoba 16 alishutumu "uhalifu usiosamehewa kwa Jamhuri", mwishoni mwa sherehe rasmi ya kumbukumbu ya miaka 60 ya mauaji ya Waalgeria yaliyofanyika Oktoba 17, 1961.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wakati wa sherehe ya kutoa heshima kwa wahanga wa mauaji ya Oktoba 17, 1961, Oktoba 16, 2021 karibu na daraja la Bezons huko Colombes, katika mkoa wa Paris.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wakati wa sherehe ya kutoa heshima kwa wahanga wa mauaji ya Oktoba 17, 1961, Oktoba 16, 2021 karibu na daraja la Bezons huko Colombes, katika mkoa wa Paris. © Rafael Yaghobzadeh, AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa "ametambua ukweli: uhalifu uliofanywa usiku huo chini ya mamlaka ya Maurice Papon hausamehewi kwa Jamhuri", imebaini taarifa kutoka Ikulu ya Elysée, ikimaanisha yule ambaye wakati wa tukio hilo alikuwa mkuu wa polisi ya Paris .

Taarifa hii ilitolewa mara tu baada ya sherehe ambayo Emmanuel Macron amehudhuria kwenye ukingo wa Seine, karibu na daraja la Bezons, lililotumiwa miaka 60 iliyopita na waandamanaji wa Algeria ambao wamiwasili kutoka makazi duni ya Nanterre huko Paris, kufuatia wito wa tawi la chama cha FLN lililoanzishwa nchini Ufaransa.

Hii ni mara ya kwanza kwa rais wa Ufaransa kuzuru eneo la mauaji hayo. Idadi ya vifo inakadiriwa na wanahistoria kuwa angalau mamia ya watu waliouawa, lakini ripoti rasmi inabaini atu watatu tu ndio waliuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.