Pata taarifa kuu
UFARANSA

Vita vya Algeria: Macron "aomba radhi " kwa jamii ya Harkis kwa niaba ya Ufaransa

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron "ameomba radhi" kwa niaba ya Ufaransa kwa jamii ya Harkis, wapiganaji kutoka jamii ya Waislamu waliosaidia jeshi la Ufaransa wakati wa Vita vya Algeria, akitangaza kupitishwa hivi karibuni kwa sheria ihusuyo "fidia".

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameahidi "kabla ya mwisho wa mwaka huu kuwasilisha mradi unaolenga kupitisha sheria inayotambua kazi kubwa iliyofanywa na jamii ya Harkis na fidia kwa jamii hii".
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameahidi "kabla ya mwisho wa mwaka huu kuwasilisha mradi unaolenga kupitisha sheria inayotambua kazi kubwa iliyofanywa na jamii ya Harkis na fidia kwa jamii hii". AP - Gonzalo Fuentes
Matangazo ya kibiashara

"Kwa wapiganaji, nataka kusema tunatambuwa kazi kubwa walioifanya kwa niaba ya Ufaransa; hatutasahau. Ninaomba radhi, hatutasahau," amesema rais Macon wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu kwa wahanga hao katikaIkulu ya Elysee, sherehe ambazo baadhi ya wapiganaji wa zamani kutoka jamii hiyo ya Harkis, viongozi wa vyama vya kiraia na viongozi mbalimbali wamehudhuria.

Ameahidi "kabla ya mwisho wa mwaka huu kuwasilisha mradi unaolenga kupitisha sheria inayotambua kazi kubwa iliyofanywa na jamii ya Harkis na fidia kwa jamii hii".

"Kwa wapiganaji, nataka kusema tunatambuwa kazi kubwa walioifanya kwa niaba ya Ufaransa; hatutasahau. Ninaomba radhi, hatutasahau," amesema rais Macon wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu kwa wahanga hao katika Ikulu ya Elysee
"Kwa wapiganaji, nataka kusema tunatambuwa kazi kubwa walioifanya kwa niaba ya Ufaransa; hatutasahau. Ninaomba radhi, hatutasahau," amesema rais Macon wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu kwa wahanga hao katika Ikulu ya Elysee Gonzalo Fuentes POOL/AFP

"Tuatendelea kuenzi kazi kubwa iliyofanywa na jamii ya Harkis", ameongeza, akitoa wito wa "kufikiria vidonda" ambavyo vyatakiwa "kuponywa kwa maneno ya ukweli, ishara za kumbukumbu na matendo ya haki".

Harkis ni wapiganaji wa zamani - ambao idadi yao ilifikia hadi 200,000 - ambao waliajiriwa kama wasaidizi wa jeshi la Ufaransa wakati wa mzozo kati ya wazalendo wa Algeria na Ufaransa kati ya mwaka 1954 na 1962.

Mwisho wa vita hivi, baadhi yao, waliotelekezwa na Paris, na kuwa waathiriwa kufuatia ulipizaji kisasi huko Algeria.

Harkis ni wapiganaji wa zamani - ambao idadi yao ilifikia hadi 200,000 - ambao waliajiriwa kama wasaidizi wa jeshi la Ufaransa wakati wa mzozo kati ya wazalendo wa Algeria na Ufaransa kati ya mwaka 1954 na 1962.
Harkis ni wapiganaji wa zamani - ambao idadi yao ilifikia hadi 200,000 - ambao waliajiriwa kama wasaidizi wa jeshi la Ufaransa wakati wa mzozo kati ya wazalendo wa Algeria na Ufaransa kati ya mwaka 1954 na 1962. Jean-Marie HURON AFP/File

Makumi kadhaa ya maelfu ya baadhi yao,  wakiongozana na wanawake na watoto, walihamishiwa nchini Ufaransa, ambako waliwekwa katika "kambi " wakiishi katika mazingira mabaya na ya kutisha.

Harkis na vizazi vyao  leo wanaunda jamii ya watu laki kadhaa nchini Ufaransa.

Walipata ujumuishaji mgumu nchini Ufaransa, wote wakifanana na wahamiaji na kukataliwa na wahamiaji.

Mnamo mwaka 2000, rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika aliwaita kama "washirika" na, wakati akikosoa mazingira ambamo wanaishi nchini Ufaransa, alikataa wasirejee nchini Algeria, akisema "sio nchi yao".

Baadhi ya wapiganaji wa zamani kutoka jamii hiyo ya Harkis, viongozi wa vyama vya kiraia na viongozi mbalimbali wamehudhuria sherehe hizo.
Baadhi ya wapiganaji wa zamani kutoka jamii hiyo ya Harkis, viongozi wa vyama vya kiraia na viongozi mbalimbali wamehudhuria sherehe hizo. AP - Gonzalo Fuentes
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.