Pata taarifa kuu
ALGERIA-UFARANSA-USHIRIKIANO

Algeria yazika wapiganaji wake waliopigana vita dhidi ya ukoloni

Algeria imezika mabaki ya wapiganaji wake 24 waliopambana na wakoloni wa Ufaransa kabla ya  nchi hiyo ya Afrika Kaskazini kupata uhuru wake miaka 58 iliyopita.

Wahanga hao waliuawa mwanzoni mwa karne ya 19 na askari wa Ufaransa ambao walikuja kutawala nchi yao. Walipigana kwa nguvu zao kutetea uhuru wa Algeria.
Wahanga hao waliuawa mwanzoni mwa karne ya 19 na askari wa Ufaransa ambao walikuja kutawala nchi yao. Walipigana kwa nguvu zao kutetea uhuru wa Algeria. Roy ISSA / AFP / Algerian TV
Matangazo ya kibiashara

Wiki iliyopita,Ufaransa iliamua kurejesha mabaki hayo ambayo sasa yamezikwa kwa heshima katika makaburi ya mashujaa.

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune, mwenyewe ndiye alipokea fuvu 24 za raia wa Algeria waliouawa walipokuwa wakipigana katika vita mwanzoni mwa kipindi cha ukoloni wa Ufaransa.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, rais wa Algeria aliiambia runinga ya France 24 kuwa, nchi yake inasubiri msamaha kutoka kwa Ufaransa baada ya nchi hiyo kutekeleza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nyakati za ukoloni.

Mabaki hayo yaliwasili nchini Algeria siku ay Ijumaa Julai 3 mchana baada ya kurejeshwa na Ufaransa kufuatia ombi rasmi lililotolewa na viongozi wa Algeria mwaka wa 2018.

Mabaki hayo, ikiwa ni pamoja na fuvu - za viongozi 24 na wapiganaji wenzao ambao walipambana dhidi ya jeshi la Ufaransa kwa kutafuta uhuru yalisafirishwa na ndege ya kijeshi ya Ufaransa hadi nchini Algeria.

Wahanga hao waliuawa mwanzoni mwa karne ya 19 na askari wa Ufaransa ambao walikuja kutawala nchi yao. Walipigana kwa nguvu zao kutetea uhuru wa Algeria.

Kati ya mwaka wa 1838 na 1865, vita dhidi ya udhibitii wa Ufaransa ilisababisha vifo vingi kwa upande wa Algeria. Wapiganaji jasiri waliuawa kwa kupigwa risasi na wakoloni, kisha miili yao kukatwa katwa na jeshi la Ufaransa kwa kulipiza kisasi.

Algeria ilipata uhuru kutoka mikononi mwa utawala wa kikoloni wa Ufaransa Julai 3, 1962.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.