Pata taarifa kuu
ALGERIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Kwa nini Algeria ni moja wapo ya nchi zilizoathirika zaidi barani Afrika

Algeria imerikodi karibu visa 8,700 vya maambukizi ya virusi vya Corona, na zaidi ya watu 600 wamefariki dunia kutokana na Covid-19. Wagonjwa 4,918 wamepona.

Zoezi la kutoa barakoa katika mji wa Algiers, Mei 21, 2020.
Zoezi la kutoa barakoa katika mji wa Algiers, Mei 21, 2020. RYAD KRAMDI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata kama idadi ya vifo hivyo iko chini kuliko vile vinarekodiwa katika mataifa mengine, takwimu hizi huiweka kwenye nafasi ya tatu ya nchi zilizoathiriwa na Corona barani Afrika. Afrika Kusini ndio inaoongoza na kufuatia na Misri.

Maelezo ya kwanza ya hali ya afya nchini Algeria yanatokana na uhusiano wa nchi hiyo na Ulaya, kwa sababu za kiuchumi na kihistoria. Algeria inapakana kwa upande wa pili wa bara la Ulaya na nchi za mwambao wa Kaskazini mwa bahari ya Mediterranian - Ufaransa, Italia, Uhispania -, ambazo pia zimeathiriwa sana na janga hilo.

Kama ilivyo nchini Morocco na Tunisia, kesi za kwanza zilizothibitishwa katika ardhi ya Algeria mwishoni mwa mwezi wa Februari ziliingizwa kutoka bara la Kale na wafanyakazi kutoka Ulaya au raia wa Algeria ambao wanaishi katika nchi za kigeni.

Karibu watu 16 wa familia moja kutoka Wilaya ya Blida, Kusini-Magharibi mwa mji mkuu wa Algiers, wameambukizwa. Eneo hilo pia limekuwa kitovu cha janga Covid-19.

Sehemu nyingine ya maelezo ili kuelewa idadi ya visa vya maambukizi vilivyorekodiwa katika nchi, ni pamoja na uwezo wake wa kufanya vipimo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.